" TIMU YA BWENI YAIFUNGA TUNGAMAA, ROBO FAINALI AWESO VIJANA CUP

TIMU YA BWENI YAIFUNGA TUNGAMAA, ROBO FAINALI AWESO VIJANA CUP

NA: MWANDISHI WETU, PANGANI 

Timu kutoka Kata ya Bweni imefanikiwa kuifunga timu ya Kata ya Tungamaa kwa ushindi wa (1-0), mechi iliyochezwa Aprili 29, 2026, katika uwanja wa Kikokwe, Kata ya Bweni, wilayani Pangani mkoani Tanga.

Katika mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa, timu ya Bweni ilipata goli kupitia kwa mchezaji wake Marino Junior katika dakika ya 35 ya mchezo, jambo lililoiwezesha Bweni kuondoka na alama tatu muhimu.

Mratibu wa mashindano hayo, Ramadhani Kibendera amesema mashindano ya Aweso Vijana Cup yamevuka matarajio kwani wananchi wanajitokeza kwa wingi viwanjani na kila timu inacheza kana kwamba inacheza fainali.

Sambamba na hilo, Kibendera amesema ligi ni ya kipekee kwani haki na sheria za mpira wa miguu zinazingatiwa na waamuzi. 

"Kwa kweli ligi ni moto, tangu ligi ianze, hamasa ni kubwa na katika jambo ambalo limekuwa nguzo kubwa ya ligi hii ni uzingatiaji wa sheria na kanuni za mchezo wa mpira wa miguu, na hakujatokea malalamiko yeyote tangu ligi izinduliwe Aprili 4, 2026," amesisitiza Kibendera.

Aweso Vijana Cup ni mashindano yanayoratibiwa na Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi ((UVCCM) wilaya ya Pangani huku Mbunge wa Jimbo hilo na Waziri wa Maji, Jumaa Aweso akiwa ndiye mdhamini wa mashindano hayo.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post