" WATANZANIA WALIUMIZWA NA GHASIA ZA 2025, TUSIKUBALI KURUDISHWA NYUMA

WATANZANIA WALIUMIZWA NA GHASIA ZA 2025, TUSIKUBALI KURUDISHWA NYUMA

 

Siku moja baada ya kutolewa kwa ripoti ya Tume ya Uchunguzi wa matukio yaliyotokea wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2025 hali ni shwari nchini.

 Watanzania wanaendelea na shughuli zao.

Mamilioni kwa mamilioni waliofuatilia uwasilishwaji wa ripoti na mapendekezo yake wanayo matumaini ya kusonga mbele kuonesha kuumizwa na ghasia zilizotokea wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu 2025. 

Hata hivyo, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) pamoja na ACT Wazalendo vimejitokeza kuipinga kazi iliyofanywa na Tume hiyo. Hata hivyo, hoja wanazozitoa zinaonekana kuwa dhaifu, hasa tukizingatia mustakabali wa nchi yetu na madhara tuliyoyapitia. 

Ni muhimu kujiuliza: kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2025, hali ya nchi ilikuwa shwari. Mambo yalianza kubadilika pale chokochoko za kupandikiza chuki na kuandaa ghasia zilipoanza kushika kasi. Kwa mujibu wa taarifa ya uchunguzi iliyotolewa jana, uratibu wa ghasia hizo ulianza takribani miezi sita kabla ya uchaguzi kufanyika.

 Baada ya kupita kwa kipindi hicho cha ghasia - ambacho ripoti imeeleza bayana kuwa ghasia hizo zilipangwa, zilifadhiliwa na kutekelezwa na watu waliopata mafunzo - Watanzania walio wengi walitamani kurejea katika amani yao waliyoizoea. Hawakutaka tena kutumika kama nyenzo ya wanasiasa kwa maslahi yao binafsi.

Baada ya kutolewa kwa ripoti, amani na utulivu vikiendelea kutamalaki, CHADEMA na ACT Wazalendo wametoa matamko yao kwa umma wakieleza sababu mbalimbali za kupinga ripoti hiyo. 

Katika taarifa yake, CHADEMA imedai kuwa kwa mujibu wa Sheria ya Uchunguzi (Commissions of Inquiry Act, 2002; Sura ya 32 kama ilivyorekebishwa mwaka 2023), Tume ni chombo cha Rais kinachofanya kazi kwa matakwa na maelekezo yake.

 Kwa mantiki hiyo, wamejaribu kuuaminisha umma kuwa Tume si chombo huru na hakiwezi kutoa ukweli wala haki, hasa katika mazingira ambayo serikali ndiyo wanayoituhumu.

Hoja wanayoieneza inahitaji ufafanuzi wa kisheria. Ni kweli kwamba Rais, kama Mkuu wa Nchi na Amiri Jeshi Mkuu, ana mamlaka ya kuunda Tume kwa mujibu wa Ibara ya 36(2) ya Katiba na Kifungu cha 3 cha Sheria ya Uchunguzi. 

Lakini kwa kutambua kuwa Tume ni chombo cha nchi, kifungu cha 6 cha Sheria ya Uchunguzi kinaweka bayana kuwa Tume haitakoma wala kuathiriwa kwa namna yoyote kutokana na kifo, kutokuwepo au kuondolewa madarakani kwa Rais aliyeiunda. Hii ni kinga muhimu ya kisheria inayolinda uhuru wa Tume katika kutekeleza majukumu yake.

Zaidi ya hapo, vifungu vya 9, 11 na 12 vya Sheria hiyo vinaipa Tume mamlaka ya kufanya kazi kwa uhuru, kujiwekea kanuni za uendeshaji wa kazi zake, na hata kutumia mamlaka ya Mahakama Kuu katika kuita mashahidi na kuhitaji taarifa zozote muhimu kwa uchunguzi wake. Hivyo basi, madai ya CHADEMA kuhusu ukosefu wa uhuru wa Tume ni upotoshaji mkubwa.

Ni muhimu pia kukumbuka kuwa CHADEMA walisusia uchaguzi, na pia hawakujitokeza mbele ya Tume.

 Leo hii wanajaribu kuibua hoja nyingine mpya, jambo linalopaswa kueleweka mapema na Watanzania wapenda amani ili wasipotoshwe.

Kwa upande mwingine, ACT Wazalendo nao wameikataa ripoti hiyo kwa hoja zinazofanana - wakidai kuwa Tume haina uhuru na iliundwa kulinda wahusika badala ya kutoa haki. 

Hoja hii inakosa mashiko pia, ukizingatia taarifa imegusia mambo mbalimbali, yakiwemo masuala yanayohitaji uwajibikaji.

Ni wazi kuwa CHADEMA na ACT Wazalendo ni wadau muhimu katika siasa za Tanzania. 

Hata hivyo, katika hatua hii, wanaonekana kuyumba baada ya kuona kuwa mkakati wa chuki waliouanzisha haukuzaa matokeo waliyotarajia.

 Aidha, kwa kususia mchakato wa Tume, wamejinyima wenyewe fursa ya kusikilizwa.

Ikumbukwe kuwa Mwenyekiti wa Tume, Jaji Mohamed Chande Othman, alieleza wazi kuwa Tume iliwafikia zaidi ya watu 63,000 na ilitoa fursa kwa kila mtu au taasisi iliyotaka kushiriki kufanya hivyo bila kikwazo. 

Wapo waliochagua kutoshiriki, wakiwa na matarajio kwamba wangeendelea kushinikiza ili vyombo vingine wanavyovitaka wao vije kufanya uchunguzi huo nchini.

Hata hivyo, wawakilishi wa taasisi za kimataifa, ikiwemo Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya Madola, tayari wamefika nchini na kuahidi kushirikiana na Tanzania katika hatua hii ya kitaifa. Hivyo basi, hoja ya kutaka kupuuzwa kwa mchakato uliopo haina msingi.

Kwa kuwa nia ya baadhi ya wanasiasa hawa inaonekana kuendelea kuwatumia Watanzania kwa maslahi ya kisiasa, ni muhimu kwa wananchi kuendelea kuwa macho na kuwakataa.

 Changamoto tuliyoipitia isijirudie tena.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post