Wanawake wajawazito wametakiwa kuepuka safari ndefu za mabasi wanapokuwa karibu kujifungua ili kujiepusha na madhara yanayoweza kuhatarisha maisha yao pamoja na watoto wanaowatarajia.Elimu hiyo imetolewa na Askari Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga, Sajenti David Ndimila, alipokuwa akizungumza na wasafiri ndani ya Stendi Kuu ya Mabasi Mkoa wa Shinyanga.Sajenti Ndimila amesema wanawake wajawazito wanaosafiri wakiwa karibu kujifungua hukabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo kujifungua ghafla ndani ya basi pasipo uwepo wa wakunga au vifaa tiba vya kumsaidia mama na mtoto.Aidha amesema mashimo yaliyopo barabarani pamoja na mitikisiko ya mabasi vinaweza kuhatarisha afya ya mama mjamzito, huku kukaa muda mrefu bila kutembea kukiongeza hatari ya damu kuganda miguuni.Pia ameeleza kuwa baadhi ya wanawake wajawazito hukumbana na changamoto ya msongo wa mawazo na unyanyasaji wanapokuwa safarini, hasa pale mabasi yanapokuwa yamejaa na kulazimika kusimama au kukosa nafasi nzuri ya kukaa.Kutokana na hali hiyo, Sajenti Ndimila amewataka wananchi kuendelea kutoa elimu hiyo katika ngazi ya familia ili kusaidia kulinda afya na usalama wa mama mjamzito pamoja na mtoto anayetarajiwa kuzaliwa.Sambamba na hilo, wanawake wajawazito wameshauriwa kutumia magari binafsi au usafiri wenye mazingira rafiki zaidi wanapokuwa karibu kujifungua ili kupunguza hatari zinazoweza kujitokeza wakiwa safarini.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254




Post a Comment