" HALMASHAURI YA MJI KASULU YAINGIA MKATABA WA MATUMIZI YA ARDHI NA MKANDARASI WA SGR, WANANCHI KUNUFAIKA ZAIDI NA MRADI HUO

HALMASHAURI YA MJI KASULU YAINGIA MKATABA WA MATUMIZI YA ARDHI NA MKANDARASI WA SGR, WANANCHI KUNUFAIKA ZAIDI NA MRADI HUO


Halmashauri ya Mji Kasulu imeingia mkataba wa matumizi ya eneo la ardhi na Mkandarasi wa Ujenzi wa Reli ya Mwendo Kasi (SGR) kwa ajili ya uzalishaji wa matofali katika eneo lenye ukubwa wa heka tano lililopo Shule ya Sekondari Kigoma Grand, Kata ya Msambala, Mtaa Mgongo.Hafla ya utiaji saini wa makubaliano hayo imefanyika katika ukumbi mdogo wa mikutano wa Halmashauri hiyo.Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Katibu Tawala wa Wilaya hiyo, Theresia Mtewele amesema Serikali itaendelea kuunga mkono juhudi za serikali katika kufanikisha mradi huo huku akiwataka wakandarasi kushirikiana kwa ukaribu na Ofisi ya Mkurugenzi wanapokutana na changamoto mbalimbali ili kurahisisha utekelezaji wake.“Matamanio yetu ni kuona shughuli hizi zinaenda vizuri, hivyo mtakapokumbana na changamoto yoyote mshirikiane na ofisi zetu ili tuweze kupata suluhisho kwa haraka” Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Ayubu Ngalaba amesema mradi huo utqchochea maendeleo ya eneo hilo na kuwanufaisha zaidi wananchi kupitia kazi zitakazotolewa.“Hatujachelewa, bado tupo kwenye muda sahihi wa kufaidika na fursa zinazotokana na mradi huu" Naye Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo  Mwl. Vumilia J. Simbeye ameishukuru Serikali kwa kuendelea kutekeleza mradi huo ndani ya Halmashauri  akiahidi kuonyesha ushirikiano mkubwa.Kwa upande wa Mkandarasi wakiongozwa na mwakilishi wao Gan Baiwen  wameishukuru Ofisi ya Mkurugenzi kwa ushirikiano mkubwa uliowezesha kupatikana kwa eneo hilo.Mradi huo unatarajiwa kuchochea shughuli za kiuchumi pamoja na kuongeza fursa za ajira kwa wananchi wa eneo husika.

 

Post a Comment

Previous Post Next Post