Na Lydia Lugakila-Misalaba Media, MbeyaMkuu wa Wilaya ya Mbeya, Solomon Itunda, amewasili rasmi katika Uwanja wa Mwawinji kwa ajili ya kufungua mashindano ya Tulia Trust Uyole Cup 2026, yanayotarajiwa kuibua ushindani mkubwa na kuendeleza vipaji vya soka katika eneo la Uyole na maeneo jirani.Mhe. Itunda ndiye mgeni rasmi wa mchezo wa ufunguzi wa mashindano hayo, ambapo pazia linafunguliwa kwa mchezo wa Ngao ya Hisani unaozikutanisha timu za Itezi United na Chipukizi FC katika Uwanja wa Mwawinji.Ujio wa Mkuu huyo wa Wilaya unaongeza hadhi ya mashindano hayo ambayo yameendelea kuwa jukwaa muhimu la kukuza vipaji vya vijana, kuimarisha mshikamano wa jamii na kuhamasisha maendeleo ya michezo katika Mkoa wa Mbeya.Mashabiki wa soka wamejitokeza kwa wingi kushuhudia mchezo huo wa ufunguzi huku wakitarajia burudani ya hali ya juu kutoka kwa timu hizo mbili zinazowania kutwaa Ngao ya Hisani na kuanza vyema kampeni ya Tulia Trust Uyole Cup 2026.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment