Zaidi ya shilingi milioni 214 zinatarajiwa kutolewa kwa wananchi wa Halmashauri ya Mji Kasulu kupitia mikopo ya asilimia 10 inayotolewa kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu ikiwa ni robo ya tatu ya mwaka.Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa wanufaika wa mikopo hiyo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kasulu Mwl. Vumilia Julius Simbeye amesema kuwa mapato ya ndani ya Halmashauri yataendelea kupanua wigo wa utoaji wa mikopo hiyo kwa lengo la kuchochea maendeleo ya wananchi pamoja na ukuaji wa uchumi wa mji wa Kasulu.Mwl. Simbeye pia amewataka wanavikundi hao kushikamana, kuwa waaminifu na kuhakikisha wanazingatia masharti ya mikopo hiyo ili kurejesha fedha kwa wakati hatua itakayowezesha wananchi wengine kunufaika.Aidha, amewasihi wananchi kutumia wataalamu wa Halmashauri pale wanapohitaji msaada ikiwemo kuwasilisha changamoto wanazokutana nazo pamoja na kupata ushauri kuhusu namna ya kuomba kuwajengea uwezo wanufaika wa mikopo hiyo muhimu za utoaji na usimamizi.


SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254








Post a Comment