" MAADHIMISHO YA SIKU YA ZIWA VICTORIA YAIBUA MIKAKATI YA UHIFADHI WA MAZINGIRA NA USALAMA WA WAVUVI ZIWA VICTORIA

MAADHIMISHO YA SIKU YA ZIWA VICTORIA YAIBUA MIKAKATI YA UHIFADHI WA MAZINGIRA NA USALAMA WA WAVUVI ZIWA VICTORIA

Na Tonny Alphonce - Misalaba MediaMaadhimisho ya Siku ya Ziwa Victoria yameanza leo katika viwanja vya Nane Nane jijini Mwanza, huku wadau mbalimbali wa mazingira wakikutana kujadili mafanikio, changamoto na mikakati ya kulinda mazingira yanayozunguka ziwa hilo kubwa zaidi barani Afrika.Akizungumza kuhusiana na  maadhimisho hayo, Mkurugenzi wa Shirika la Usimamizi wa Mazingira na Maendeleo (EMEDO), Edtrudith Lukanga amesema maadhimisho hayo yana umuhimu mkubwa kwa kuwa yanatoa fursa kwa wadau wa mazingira kueleza kazi walizofanya na wanazoendelea kufanya katika kuhifadhi mazingira ya Ziwa Victoria.Amesema kwa mara ya kwanza maadhimisho hayo yanafanyika Mwanza, jambo ambalo limeongeza nafasi kwa wananchi, taasisi na viongozi wa serikali kukutana pamoja kujadili changamoto zinazohusu mazingira, maji pamoja na jamii zinazozunguka ziwa hilo.“Maadhimisho haya yanatupa nafasi ya kuwasilisha yale tunayofanya lakini pia kusikiliza changamoto zilizopo ili kwa pamoja tuweze kutafuta suluhisho endelevu,” amesema Lukanga.Aidha kwa upande wa Usalama Kwa watumiaji wa Ziwa,ameeleza kuwa EMEDO kwa kushirikiana na Tanzania Meteorological Authority (TMA) wamefanikiwa kuboresha usalama wa wavuvi na wafanyabiashara wanaotegemea shughuli za Ziwa Victoria kupitia huduma za utabiri wa hali ya hewa.Kwa mujibu wa Lukanga, hivi sasa wavuvi wana uwezo wa kupata taarifa za hali ya hewa moja kwa moja kutoka Dar es Salaam hadi katika visiwa wanavyofanyia shughuli zao kupitia mabango maalumu yaliyowekwa katika maeneo mbalimbali ya visiwani.Amesema mfumo huo unawasaidia wavuvi kujua hali ya ziwa kama ni salama au hatarishi kabla ya kwenda kuvua, hatua inayochangia kupunguza ajali na matukio ya kuzama maji.“Wafanyabiashara pia wanapata manufaa ya taarifa hizi kwani huwasaidia kufanya maamuzi sahihi kuhusu biashara zao, ikiwemo kununua au kutonunua dagaa kulingana na hali ya hewa inayotarajiwa,” ameongeza.Kwa upande wake, Mratibu wa Mradi wa Kuzuia Kuzama Maji Ziwa Victoria, Arthur Mgema amesema EMEDO imekuwa mstari wa mbele katika shughuli za utunzaji wa mazingira kupitia miradi mbalimbali ya uhifadhi.Mgema amesema shirika hilo kwa kushirikiana na University of Dar es Salaam lilifanya utafiti katika fukwe 69 za maziwa ya Victoria, Nyasa na Tanganyika, ambapo ripoti ya utafiti huo ilionesha kuwa taka za plastiki ndizo zilikuwa nyingi zaidi katika maeneo hayo.Mbali na kufanya utafiti huo, amesema pia walifanya kampeni za usafi katika maeneo ya fukwe kwa lengo la kuongeza uelewa wa jamii kuhusu athari za uchafuzi wa mazingira ya maji.Maadhimisho ya Siku ya Ziwa Victoria yanatarajiwa kuwakutanisha wadau mbalimbali wa mazingira, taasisi za serikali, mashirika binafsi pamoja na wananchi kwa lengo la kujadili njia bora za kuhifadhi mazingira ya ziwa hilo muhimu kwa uchumi na maisha ya mamilioni ya watu wa Afrika Mashariki.

 SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post