Na Mapuli Kitina Misalaba
Mabingwa watetezi wa mashindano ya NIACHEKONA CUP
2024, timu ya SANGU FC kutoka Wilaya ya Kwimba Mkoa wa Mwanza wameendelea
kuonesha ubabe wao baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya BULIGE FC
kutoka Msalala Wilaya ya Kahama katika mchezo wa ushindani mkubwa uliochezwa
kwenye uwanja wa Mwabenda kata ya Solwa, Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.
Baada ya mchezo huo, Katibu wa Kamati ya Mashindano
Sambayi Jilya amesema kuwa mzunguko wa kwanza wa ligi ya NIACHEKONA CUP 2026
umetamatika rasmi leo Jumanne Mei 26, 2026 ambapo kuanzia kesho timu zote
zilizocheza katika hatua ya kwanza zitaanza michezo ya marudiano ili kupata
timu zitakazofuzu kuingia hatua ya kumi na mbili bora.
Aidha Sambayi ametangaza ratiba ya mchezo wa kesho
ambapo timu ya MANHEIGANA itamenyana na HOME BOYS, timu zote kutoka kata ya
Solwa Mkoa wa Shinyanga katika mchezo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa
ndani ya mashindano hayo.
Ameendelea kuwaomba wananchi wa Solwa pamoja na maeneo
jirani kujitokeza kwa wingi katika uwanja wa Mwabenda kushuhudia michezo hiyo
ambayo imeendelea kuwa jukwaa la kuibua vipaji vya vijana kupitia soka.
Mashindano ya NIACHEKONA CUP 2026 yameandaliwa na
Bwana Paul Daud Augustino kupitia ufadhili wa shirika la Lushu Foundation kwa
lengo la kuibua vipaji vya vijana, kukuza michezo pamoja na kuimarisha
mshikamano wa jamii kupitia soka.
Kwa huduma za ushereheshaji wa shughuli mbalimbali,
matangazo pamoja na burudani unaweza kuwasiliana na MC NIACHEKONA kupitia namba
0757 267 738.
Timu ya SANGU FC
Wachezaji wa SANGU FC na BULIGE FC wakioneshana ushindani mkubwa loe Mei 26, 2026 katika ligi ya NIACHEKONA CUP 2026 inayoendelea kwenye uwanja wa Mwabenda kata ya Solwa.

Mchezo ukiendelea ambapo mabingwa watetezi SANGU FC waliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya BULIGE FC kutoka Wilaya ya Kahama.

Mashabiki wakifuatilia kwa hamasa kubwa mchezo wa SANGU FC dhidi ya BULIGE FC katika uwanja wa Mwabenda.

Awali Mabingwa watetezi wa NIACHEKONA CUP 2024, SANGU FC wakimkabidhi kombe lao kwa Mwenyekiti wa mashindano hayo kabla ya mchezo wao dhidi ya BULIGE FC katika uwanja wa Mwabenda kata ya Solwa.SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment