Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Juma Homera.Na,Egidia Vedasto,Misaaba Media, Arusha.Mafunzo Kwa Mawakili wa serikali takriban 600 yameanza kutolewa Jijini Arusha yakilenga kuwajengea uwezo na kuongeza ufanisi katika utendaji kazi wao.Akifungua mafunzo hayo Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Juma Homera amewataka Mawakili hao kuzingatia mafunzo yatakayotolewa ili yawawezeshe kuendesha mashauri ya serikali Kwa weledi.Kipekee naipongeza Ofisi ya Wakili Mkuu Kwa kazi kubwa wanayoifanya kuisaidia serikali katika kushinda kesi nyingi hatua iliyopelekea kuokoa jumla ya ahilingi Trillion 1.35, katika mkakati tuliouweka kupunguza migogoro ya ardhi, tutahakikisha mabaraza yote ya ardhi yanakuwa chini ya mahakama ili kupunguza migogoro hiyo" amesema Dkt Homera.Kwa upande wake Wakili Mkuu wa Serikali Dkt.Ally Possi ameishukuru serikali Kwa kuwawezesha Mawakili kupata mafunzo ya mara Kwa mara na kuahidi kuwa wataendelea kushughulikia mashauri na kulinda maslahi ya taifa."Tunajivunia kushinda kesi 565 Kwa kipindi cha mwaka mmoja yakiwemo mashauri ya uwekezaji na kupelekea kuokoa pesa nyingi sana. Tunaahidi Kwa weledi, maadili na uzalendo tutaendelea kuitetea serikali, na kutetea maslahi ya taifa letu linapoingia mikataba ya uwekezaji na sekta binafsi" amesema Dkt. Possi.Vile vile Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge utawala Katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro amesisitiza Mawakili kufanya kazi Kwa uadilifu na uaminifu, kutumia mashauri yanayoendeshwa kama darasa na kuhakikisha wanazingatia msingi wa Dira 2020-2050 ambayo Kwa asilimia 78% inaongelea utawala wa Sheria."Mna kazi kubwa ya kuisaidia serikali ndiyo maana mnaitwa Mawakili wasomi, endeleeni kujifunza Kila siku lakini pia isaidieni serikali kumulika wale wanaolichafua Taifa Kwa maneno ya uchochezi wa mitandaoni na wanaozusha uongo na kusababisha taharuki Kwa wananchi" ameongeza Dkt.Ndumbaro.
Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Ally Possi.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment