Na Mapuli Kitina Misalaba
Ligi ya NIACHEKONA CUP 2026 inayoendelea katika uwanja
wa Kijiji cha Mwabenda kata ya Solwa, Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
imeendelea kupamba moto ambapo timu ya DUARA FC imeibuka na ushindi mnono wa
mabao 3-0 dhidi ya MWANDUTU katika mchezo uliochezwa leo Mei 18, 2026.
Mashindano hayo yaliyoanza rasmi Mei 16, 2026
yanashirikisha jumla ya timu 22 kutoka maeneo mbalimbali ndani na nje ya Mkoa
wa Shinyanga ikiwemo Mwanza, Geita, Kahama, Manispaa ya Shinyanga pamoja na
Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga jimbo la Solwa.
Katibu wa Kamati ya Mashindano Sambayi Jilya amesema
michezo ya NIACHEKONA CUP 2026 itaendelea kesho ambapo timu ya SHILIMA kutoka
Mwanza itashuka dimbani kuivaa SONGAMBELE MHANGU katika mchezo unaotarajiwa
kuwa na ushindani mkubwa kutokana na ubora wa timu hizo.
Naye mwandaaji wa mashindano hayo Bwana Paul Daud
maarufu MC NIACHEKONA amesema mafanikio ya mashindano hayo yanatokana na
ushirikiano mkubwa kutoka kwa wananchi, wadau wa michezo pamoja na timu
zinazoshiriki ambazo zimeonesha nidhamu na ushindani wa hali ya juu tangu
kuanza kwa ligi hiyo.
Amesema dhamira yake ni kuona vijana wa Solwa na
maeneo mengine wanapata jukwaa la kuonesha uwezo wao wa kisoka huku mashindano
hayo yakizidi kuwa sehemu ya kuimarisha mshikamano, burudani na kuibua vipaji
vitakavyoweza kufika katika ngazi kubwa za soka nchini.
MC NIACHEKONA pia amewashukuru wadhamini na marafiki
mbalimbali wanaoendelea kuunga mkono mashindano hayo huku akisema mchango wao
umeendelea kusaidia kukuza michezo katika kata ya Solwa na maeneo jirani.
Amewataja baadhi ya wadau wanaoendelea kutoa
ushirikiano kuwa ni pamoja na Jambo FM kupitia kipindi cha Extra Time pamoja na
Mabula Lushulwanhambi wa Mahembe kwa mchango wao mkubwa katika kufanikisha
maendeleo ya michezo na uwanja wa Mwabenda.
Mbali na kuwa mwandaaji wa NIACHEKONA CUP 2026, Bwana Paul Daud maarufu MC NIACHEKONA pia ni Meneja wa Kishushu Hotel na mchimba madini katika mgodi wa Mwakitolyo. Kwa huduma za ushereheshaji (MC), matangazo na shughuli mbalimbali wasiliana naye kupitia namba 0757 267 738.



Viongozi mbalimbali pamoja na wadau wa michezo wakifuatilia mchezo wa NIACHEKONA CUP 2026 katika uwanja uliopo Mwabenda kata ya Solwa.
Diwani wa kata ya Solwa Mhe. Dotto Samson na mtendaji wa kata hiyo Jackson Maganga wakifuatilia mechi.
Sehemu ya mashabiki wakifuatilia kwa hamasa mchezo wa NIACHEKONA CUP 2026 uliozikutanisha DUARA FC dhidi ya MWANDUTU.

Sehemu ya mashabiki wakifuatilia kwa hamasa mchezo wa NIACHEKONA CUP 2026 uliozikutanisha DUARA FC dhidi ya MWANDUTU.

Sehemu ya mashabiki wakifuatilia kwa hamasa mchezo wa NIACHEKONA CUP 2026 uliozikutanisha DUARA FC dhidi ya MWANDUTU.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254




































Post a Comment