" MAMA LISHE WAFUNGUKA FAIDA ZA NIACHEKONA CUP, WAITAKIA UBINGWA HOME BOYS

MAMA LISHE WAFUNGUKA FAIDA ZA NIACHEKONA CUP, WAITAKIA UBINGWA HOME BOYS

Na Mapuli Kitina Misalaba

Baadhi ya Mama Lishe wanaofanya biashara katika kata ya Solwa, Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga wamefunguka kuhusu faida wanazoendelea kuzipata kupitia mashindano ya NIACHEKONA CUP 2026 huku wakiitakia timu ya HOME BOYS kutwaa ubingwa wa mashindano hayo mwaka huu.

Wakizungumza na Misalaba Media kwa nyakati tofauti, Mama Lishe hao wamesema mashindano hayo yamechangia kuongezeka kwa wateja kutokana na idadi kubwa ya mashabiki, wachezaji na wageni wanaofika kufuatilia michezo hiyo kila siku.

Wamesema tofauti na siku za kawaida, siku za mechi huwaletea fursa kubwa ya kuuza vyakula na vinywaji jambo ambalo limewaongezea kipato na kuwasaidia kuendesha maisha yao ya kila siku.

Aidha wamempongeza mwandaaji wa mashindano hayo, Bwana Paul Daud Augustino maarufu MC NIACHEKONA kwa kuendelea kuandaa mashindano yanayokuza vipaji vya vijana huku yakichochea shughuli za kiuchumi kwa wananchi wa eneo hilo.

Mama Lishe hao pia wameeleza kuvutiwa na kiwango kinachooneshwa na timu ya HOME BOYS katika mashindano hayo na kuitakia mafanikio zaidi huku wakiamini inaweza kufika hatua ya mwisho na kutwaa ubingwa wa NIACHEKONA CUP 2026.

Wameongeza kuwa mashindano hayo yanapaswa kuendelea kuungwa mkono na wadau mbalimbali kwa kuwa yana manufaa makubwa kwa vijana, wafanyabiashara na jamii kwa ujumla.

Mashindano ya NIACHEKONA CUP 2026 yanaendelea katika uwanja wa Mwabenda kata ya Solwa yakihusisha timu mbalimbali kutoka ndani na nje ya Mkoa wa Shinyanga kwa lengo la kuibua vipaji vya vijana na kukuza michezo kupitia ufadhili wa Lushu Foundation.

 SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post