" MBINGA YAPOKEA MWENGE WA UHURU 2026, MIRADI YA BILIONI 1.3 KUPITIWA

MBINGA YAPOKEA MWENGE WA UHURU 2026, MIRADI YA BILIONI 1.3 KUPITIWA

  

Na: Yusuph Kayanda – Mbinga

Wilaya ya Mbinga imepokea rasmi Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2026 kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Songea, huku Mkuu wa Wilaya ya Mbinga, Kisare Makori, akikiri kuupokea mwenge huo utakaokimbizwa umbali wa kilomita 169.5 kwa lengo la kukagua, kuzindua na kuweka mawe ya msingi kwenye miradi sita ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 1.3

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Makori amesema mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka huu zitatoa fursa ya kuonesha utekelezaji wa miradi inayolenga kuboresha huduma kwa wananchi katika sekta mbalimbali, huku akiwahimiza wakazi wa Mbinga kuishi kwa vitendo kauli mbiu ya Mwenge wa Uhuru 2026 isemayo, “Tanzania ni yetu sote, tushikamane kwa pamoja kuleta maendeleo,” kwa kudumisha mshikamano, uwajibikaji na ushiriki katika shughuli za maendeleo.

Baada ya kukimbizwa katika Wilaya ya Mbinga na kupitia miradi hiyo ya maendeleo, Mwenge wa Uhuru 2026 unatarajiwa kukabidhiwa Wilaya ya Nyasa, huku wananchi wakihamasishwa kujitokeza kushiriki shughuli za mwenge na kujionea maendeleo yanayotekelezwa katika maeneo yao.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post