" MC NIACHEKONA AWASHUKURU MASHABIKI NA WADAU WA MICHEZO SHINYANGA

MC NIACHEKONA AWASHUKURU MASHABIKI NA WADAU WA MICHEZO SHINYANGA

 

Na Mapuli Kitina Misalaba

Mkurugenzi wa mashindano ya NIACHEKONA CUP 2026 ambaye pia ni mwandaaji wa mashindano hayo Paul Daud Augustino amewashukuru watanzania pamoja na wadau mbalimbali wa michezo kwa kuendelea kufuatilia na kuunga mkono mashindano hayo yanayoendelea katika uwanja wa Mwabenda kata ya Solwa, Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.

Akizungumza na Misalaba Media, MC NIACHEKONA amesema amefurahishwa na mwitikio mkubwa wa wananchi pamoja na mashabiki wa soka ambao wamekuwa wakijitokeza kwa wingi kila siku kushuhudia michezo pamoja na vipaji vya vijana vinavyoendelea kuonekana kupitia ligi hiyo.

Aidha amewashukuru wadau mbalimbali wanaoendelea kumpa ushirikiano katika kufanikisha mashindano hayo ikiwemo Jambo FM pamoja na Misalaba Media kwa namna wanavyoendelea kutoa taarifa za michezo hiyo kwa wananchi kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.

Pia amemshukuru Mkurugenzi wa Shirika la Lushu Foundation Mabula Charles Lushu kwa mchango wake mkubwa katika kusaidia maendeleo ya michezo pamoja na vijana kupitia udhamini wa mashindano hayo.

“Naendelea kuwashukuru watanzania wote wanaoendelea kufuatilia ligi hii pamoja na wadau wote wanaonipa ushirikiano kuhakikisha mashindano haya yanaendelea kuwa bora zaidi,” amesema MC NIACHEKONA.

Mbali na shughuli za michezo, MC NIACHEKONA amewakaribisha wananchi pamoja na watanzania mbalimbali kufika katika Kishushu Hotel kwa ajili ya kupata huduma mbalimbali ikiwemo malazi, chakula pamoja na vinywaji katika mazingira mazuri na salama.

Kwa huduma za ushereheshaji wa shughuli mbalimbali, matangazo pamoja na burudani unaweza kuwasiliana na Paul Daud Augustino kupitia namba 0757 267 738.


SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post