" MICHEZO YA NIACHEKONA CUP YATAJWA KUJENGA AMANI SOLWA

MICHEZO YA NIACHEKONA CUP YATAJWA KUJENGA AMANI SOLWA

 

Na Mapuli Kitina Misalaba

Jeshi la Polisi kata ya Solwa limepongeza jitihada zinazofanywa na mdau wa michezo katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Paul Daud Augustino kwa kuanzisha mashindano ya NIACHEKONA CUP 2026 ambayo yameendelea kuwa jukwaa muhimu la kuibua vipaji vya vijana pamoja na kuimarisha amani katika jamii.

Akizungumza katika mashindano hayo yanayoendelea kwenye uwanja wa Mwabenda kata ya Solwa, Polisi Kata wa kata ya Solwa Paul Mashimba amesema michezo hiyo imekuwa na mchango mkubwa katika kuwaweka vijana karibu na shughuli za maendeleo badala ya kujihusisha na vitendo visivyofaa katika jamii.

“Kwanza kabisa namshukuru mdau wa michezo katika Wilaya hii ambaye ni MC NIACHEKONA kwa kuanzisha hii ligi na mashindano katika kata yetu. Mimi kama Polisi Kata nawaasa wananchi wote pamoja na vijana kutumia fursa hii vizuri ili waweze kuibua vipaji vyao lakini pia kufikia malengo yao waliyojiwekea katika michezo,” amesema Mashimba.

Amesema Jeshi la Polisi linaunga mkono mashindano hayo kwa kuwa michezo imekuwa njia muhimu ya kuwafanya vijana kuwa bize na shughuli zenye manufaa badala ya kukaa vijiweni na kujihusisha na matumizi ya dawa za kulevya pamoja na vitendo vya kihalifu.

“Watu wanapokuwa kwenye michezo hawawezi kuwaza mambo ya uhalifu kama uvunjaji, wizi na mambo mengine yasiyopendeza katika jamii. Michezo ni afya, michezo ni urafiki, michezo ni ujamaa lakini pia ni fursa kwa sababu watu wanatoka maeneo mbalimbali ndani na nje ya mkoa kukutana hapa,” ameongeza.

Aidha amewatahadharisha wananchi wenye nia ya kuvuruga amani au kufanya vitendo vya kihalifu wakati wa mashindano hayo kuwa sheria itachukua mkondo wake kwa yeyote atakayebainika kwenda kinyume na taratibu zilizowekwa.

Mashimba amesema mashindano ya NIACHEKONA CUP 2026 yanatambulika rasmi kuanzia ngazi ya serikali ya kijiji, serikali ya kata, kamati ya ulinzi na usalama ya kata hadi ngazi ya wilaya pamoja na Baraza la Michezo Mkoa wa Shinyanga hivyo mtu yeyote atakayevunja sheria atachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwemo kufikishwa polisi na mahakamani.

Mashindano hayo yameandaliwa na Paul Daud Augustino kupitia ufadhili wa shirika la Lushu Foundation kwa lengo la kuibua vipaji vya vijana, kuimarisha mshikamano wa jamii pamoja na kukuza michezo katika Mkoa wa Shinyanga.

Kwa huduma za ushereheshaji wa shughuli mbalimbali, matangazo pamoja na burudani unaweza kuwasiliana na Paul Daud Augustino kupitia namba 0757 267 738.

 SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post