" MISA TANZANIA KANDA YA KASKAZINI YAIMARISHA USHIRIKIANO NA EWURA

MISA TANZANIA KANDA YA KASKAZINI YAIMARISHA USHIRIKIANO NA EWURA

Na.Mwandishi wetu ArushaTaasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA Tanzania) kupitia Kanda ya Kaskazini, leo Mei 05, 2026, imetembelea ofisi ya Kanda ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati (EWURA) Jijini Arusha na kufanya mazungumzo na Meneja wa Kanda kwa lengo la kuimarisha ushirikiano baina ya taasisi hizo mbili.Katika ziara hiyo, ujumbe wa MISA Tanzania ulioongozwa na Mwenyekiti wake, Edwin Soko na baadhi ya wanachama wa MISA wa Kanda ya Kaskazini, ulikutana na Meneja wa EWURA Kanda ya Kaskazini, George Muhina, ambapo walijadiliana namna ya kushirikiana katika kuhabarisha umma kuhusu masuala ya maji na nishati pamoja na majukumu ya EWURA.Akizungumza wakati wa kikao hicho, Meneja wa EWURA Kanda ya Kaskazini, Bwana Muhina, ameipongeza MISA Tanzania na wanachama wake kwa juhudi zao za kuandika habari zenye ubora kuhusu shughuli za EWURA, Pia alisema hatua  hiyo inachangia kuongeza uelewa wa jamii kuhusu majukumu ya mamlaka hiyo. Alieleza kuwa uwepo wa waandishi vinara wa habari za maji na nishati waliopata mafunzo kutoka EWURA Makao Makuu umeongeza weledi katika uandishi wa habari hizo.Aidha, Bwana Muhina aliwahimiza waandishi wa habari kuendelea kujenga utamaduni wa kupitia na kutumia ripoti mbalimbali zinazotolewa na EWURA ili kuhakikisha taarifa sahihi na zenye tija zinawafikia wananchi kwa wakati.Kwa upande wake, Mwenyekiti wa MISA Tanzania, Bwana Soko, alieleza kuwa EWURA ina jukumu kubwa na la msingi katika kudhibiti huduma za maji na nishati nchini, hivyo MISA Tanzania itaendelea kuwa mdau muhimu kwa kushirikiana na EWURA katika kuelimisha umma na kuimarisha uwajibikaji kupitia vyombo vya habari.Ziara hiyo ni sehemu ya mkakati wa MISA Tanzania wa kuimarisha mahusiano na wadau mbalimbali katika kanda, kwa lengo la kukuza taaluma ya habari na kuhakikisha upatikanaji wa taarifa sahihi kwa jamii.

 SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post