Abiria wanaosafiri kwenda minadani wamepatiwa elimu ya usalama barabarani kuacha kupanda Bajaji za mizingo ili kuepukana na ajali za mara Kwa mara barabarani.
Elimu hiyo imetolewa na Askari Polisi wa Kikosi Cha usalama barabarani Mkoa wa Shinyanga Sajenti David Ndimila katika barabara ya Old Shinyanga ambapo amewaeleza abiria kuwa Bajaji ya mizigo sio usafiri salama kwao na haina mazingira rafiki kulinda usalama wao hivyo kuacha tabia ya kupanda usafiri huo wa kubebea mizigo badala yake kutafuta usafiri unaoruhusiwa kubeba abiria.
Sajenti Ndimila amewaeleza abiria hao kuwa kupanda bajaji ya mizigo ni hatari sana na inaweza kusababisha madhara makubwa kwao pindi ajali inapotokea.
Aidha abiria hao wameaswa kujitambua na kuacha kurubuniwa kupanda katika usafiria huo kwani dereva wa chombo husika anaangalia maslahi binafsi na sio usalama wao.


SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment