Ushirikishwaji hafifu na hisia za kutosikilizwa zimetajwa kuwa miongoni mwa vichocheo vilivyowafanya baadhi ya vijana kujitenga na mifumo halali ya kidemokrasia na kujiingiza kwenye propaganda wakati wa Uchaguzi Mkuu wa 2025.
Hilo limebainika kupitia Ripoti ya Tume ya Jaji Mohamed Chande Othman, ambayo imesisitiza haja ya kujenga mifumo mipya ya kusikiliza sauti za vijana mapema.
Ripoti inaeleza kuwa vijana wengi waliohojiwa walionesha hisia za kutokuwakilishwa kikamilifu katika mijadala mikubwa ya kisiasa na kijamii, jambo lililowafanya baadhi yao kuamini kaulimbiu za 'mabadiliko' ya vurugu kupitia mitandao ya kijamii.
Ili kurekebisha hali hii, tume imependekeza kuwepo kwa mikakati madhubuti ya kutoa elimu ya uraia ili kujenga kizazi kinachoweza kuchambuzi taarifa kwa umakini na kushiriki siasa kwa njia za amani.
Hata hivyo, Jaji Chande aligusia kuwa wananchi na vijana wengi waliofika mbele ya tume hiyo bado wana matumaini makubwa na mustakabali wa Tanzania, wakitamani kuona taifa linarudi kwenye misingi ya amani, umoja na mshikamano.
Ili kufikia lengo hilo, ripoti imetoa wito wa kuongezwa kwa nafasi za vijana katika uongozi, ubunifu, na mijadala ya sera ili wawe nguzo ya maendeleo badala ya kuwa chombo cha migogoro.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment