Mkuu wa Idara ya Utamaduni, Makongamano na Utalii
Taifa, Shujaa Daniel Kapaya, amewataka Mashujaa wote nchini kuanzia ngazi ya
mkoa, wilaya hadi kata kushiriki kikamilifu katika maadhimisho ya Siku ya
Makumbusho ya Utamaduni Duniani kwa kutembelea makumbusho na vivutio vya utalii
wa kitamaduni vilivyopo karibu nao.
Akitoa taarifa hiyo, Kapaya amesema maadhimisho hayo
yatafanyika Mei 18, 2026, yakilenga kuhamasisha wananchi kujifunza historia,
mila na desturi za jamii mbalimbali pamoja na kukuza utalii wa ndani.
Amesema kauli mbiu ya mwaka huu ni; “Tembelea
Makumbusho, Jifunze Historia Yetu, Hamasisha Utalii wa Ndani, Linda Jamii Dhidi
ya Ukatili wa Kijinsia.”
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, baadhi ya maeneo
yatakayohamasishwa kutembelewa ni pamoja na Makumbusho ya Taifa na Nyumba ya
Utamaduni ya Dar es Salaam, Village Museum, Makumbusho ya Mwalimu Nyerere
Butiama, Bujora Cultural Centre ya Mwanza, Bagamoyo Museum, Chagga Museum,
pamoja na Makumbusho ya Utumwa Zanzibar.
Kapaya amesema pia wananchi wanaruhusiwa kutumia
vyombo mbalimbali vya habari kufanya midahalo na kutoa elimu kuhusu mila,
desturi, utamaduni na umuhimu wa utalii wa ndani kwa maendeleo ya taifa.
Aidha, amesisitiza kuwa kila mkoa unapaswa kutumia
fursa hiyo kutangaza maeneo yake ya kihistoria na kiutamaduni yaliyopo ndani ya
maeneo yao hata kama hayajatajwa rasmi katika orodha ya kitaifa.
Taarifa hiyo imetolewa na Kurugenzi ya Makongamano,
Utalii na Utamaduni Taifa.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment