" MWENYEKITI UWT KATAVI AFANYA ZIARA KATA 19 MPANDA, ASISITIZA UMOJA NA UHAI WA JUMUIYA

MWENYEKITI UWT KATAVI AFANYA ZIARA KATA 19 MPANDA, ASISITIZA UMOJA NA UHAI WA JUMUIYA


Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Tanzania Mkoa wa Katavi, Fortunata Kabeja, amefanya ziara katika kata 19 za Wilaya ya Mpanda Aprili 5, 2026, akikutana na wanachama wa jumuiya hiyo pamoja na Chama Cha Mapinduzi kwa lengo la kuimarisha uhai wa jumuiya na mshikamano.

Katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa CCM Wilaya ya Mpanda, Kabeja aliwasalimia wanachama na kuwakumbusha umuhimu wa kuwa na mawazo chanya ya kujenga jumuiya na chama kwa kushirikiana, kufanya mikutano ya mara kwa mara na kupeana maelekezo ya kiutendaji.

Aidha, aliwashukuru wanachama kwa mchango wao mkubwa uliopelekea ushindi wa chama katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 katika ngazi mbalimbali, ikiwemo madiwani, wabunge na nafasi ya urais.

Akizungumzia uhai wa jumuiya, Kabeja aliwataka wanachama kuongeza juhudi katika kulipa ada na kuandikisha wanachama wapya ili kuimarisha jumuiya hiyo katika ngazi za mashina, matawi, kata na wilaya.

Katika hatua nyingine, aliahidi kutoa vyeti vya shukrani kwa kata zitakazofanya vizuri kama njia ya kuhamasisha utendaji bora, huku akisisitiza umuhimu wa umoja na mshikamano bila kubaguana.

Pia aliwataka wanachama kuendeleza upendo, amani na kuheshimiana katika utekelezaji wa majukumu ya jumuiya na chama, akibainisha kuwa maadili hayo ni msingi wa maendeleo na mafanikio ya pamoja.

Kabeja aliwahamasisha wanawake kujihusisha na shughuli za ujasiriamali na kubuni miradi midogo midogo itakayowaongezea kipato, sambamba na kuzingatia maadili ya nidhamu, uaminifu, uzalendo na ushirikiano.

Katika ziara hiyo, aliwataka viongozi wa ngazi mbalimbali kuhakikisha wanakuwa na takwimu sahihi za wanachama, kufanya vikao vya mara kwa mara, kutunza kumbukumbu, kusikiliza na kutatua kero za wanachama kwa wakati.

Ziara hiyo ilihitimishwa kwa maelekezo kwa viongozi wa mashina, matawi, kata na wilaya kuendelea kusimamia majukumu yao kwa uwajibikaji, huku wakisisitizwa kubuni miradi ya maendeleo, kuimarisha mawasiliano na kujenga mahusiano mazuri kati ya chama na serikali.

Ziara hiyo ilihusisha kata mbalimbali zikiwemo Kashaulili, Majengo, Misunkumilo, Nsemulwa, Kakese, Ibindi, Sitalike na Itenka, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuimarisha Jumuiya ya UWT na chama kwa ujumla katika Mkoa wa Katavi.

Ndg. Fortunata Kabeja, Mwenyekiti wa Jumuiya ya UWT Mkoa wa Katavi, akisaini kitabu cha wageni alipowasili Wilaya ya Mpanda.

Ndg. Taus, Mwenyekiti wa Jumuiya ya UWT Wilaya ya Mpanda, akiwasalimia na kuwakaribisha wajumbe kwenye kikao, kisha akakifungua na kuwaomba wajumbe kuwa na utulivu kumsikiliza Ndg. Fortunata Kabeja, Mwenyekiti wa Jumuiya ya UWT Mkoa wa Katavi.

Ndg. Mary, Katibu wa Jumuiya ya UWT Mkoa wa Katavi, akiwasalimia na kuwakaribisha wajumbe katika kikao cha ziara ya Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo mkoani Katavi.

Ndg. Jimotoli Jilala Maduka, Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi, ambaye pia ni Kaimu Katibu wa Jumuiya ya UWT Wilaya ya Mpanda, ameshiriki kikamilifu katika kikao cha ziara ya Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Katavi, Ndg. Fortunata Kabeja, kilichofanyika katika Wilaya ya Mpanda.Ndg. Jimotoli Jilala Maduka, Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi, ambaye pia ni Kaimu Katibu wa Jumuiya ya UWT Wilaya ya Mpanda, ameshiriki kikamilifu katika kikao cha ziara ya Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Katavi, Ndg. Fortunata Kabeja, kilichofanyika katika Wilaya ya Mpanda.Mh. Anna Joseph Mayaya, Diwani Viti Maalum wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda (Tarafa ya Misunkumilo) na Mjumbe wa Baraza Kuu la UWT Taifa, ameshiriki kikamilifu katika kikao cha ziara ya Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Katavi, Ndg. Fortunata Kabeja, kilichofanyika Wilaya ya Mpanda, akisisitiza umuhimu wa umoja na mshikamano pamoja na ubunifu wa miradi ya maendeleo kwa wanachama wa jumuiya.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254




 

Post a Comment

Previous Post Next Post