Na mwandishi wetu,Mbeya
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya, linawashikilia watu saba kwa tuhuma za kujipatia Shilingi Milioni 81 kwa njia za udanganyifu wa kuwarubuni Vijana 80 kuwa watawapatia ajira ndani na nje ya Tanzania kupitia makampuni ya Q Net na Global Alliance.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Benjamin Kuzaga amesema watuhumiwa hao wamekamatwa Alhamisi Mei 14,2026, kwenye msako uliofanywa katika maeneo mbalimbali jijini hapa.
"Watuhumiwa walikuwa wakiwashawishi vijana watoe kiasi cha Shilingi 40, 000 hadi Shilingi milioni 5 kwa lengo la kuwapatia ajira katika kampuni hiyo." amesema Kamanda Kuzaga.
Amesema kufuatia udanganyifu huo zaidi ya vijana 80 waliingia kwenye mtego na kukusanywa katika nyumba tofauti maeneo ya Iwambi, Shewa, Isyesye na Iyunga halmashauri ya Jiji la Mbeya.
Kamanda Kuzaga amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Willam Hamis, Tyson Lubida, Onesmo Haldphonce, Charles Masanja, Chemka Mwanyanga, Gracia Ephrahim, wote wakati wa jijini Mbeya na Ezekiel Mgogo mkazi wa Igunga Mkoa wa Tabora.
"Watuhumiwa walitumia mbinu ya kuwarubuni vijana kutoka mikoa mbalimbali kuwaleta mkoani hapa kwa lengo kuwapatia ajira jambo ambalo sio sahihi na kupelekea kuishi maisha ya shida kwa kukosa huduma," amesema.
Wakati huohuo, Kamanda Kuzaga amewaonya vijana kuepuka kutafuta ajira kwa kutakiwa kutanguliza fedha na badala yake watumie mifumo rasmi .
"Vijana mnaotafuta ajira msikubali kutoa fedha ili kupata ajira kwani hakuna utaratibu huo na badala yake kutoa taarifa kwa vyombo vya dola ili kujinasua kwenye mitego," amesema.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment