Mbunge wa Jimbo la Kasulu Mjini Profesa Joyce Ndalichako, amekabidhi viti mwendo 10 kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu katika Shule ya Msingi Kalema iliyopo Halmashauri ya Mji Kasulu kwa lengo la kuboresha mazingira yao ya kujifunzia.Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Profesa Ndalichako amesema ataendelea kushirikiana na viongozi wa Halmashauri ya Mji Kasulu kuhakikisha watoto wenye ulemavu wanapata mazingira bora ya elimu."Hii kwa kweli ni baraka na baraka hii nitaendelea kuitafuta kwa hali na mali kwa kadri Mungu atakavyonijalia nitawashika mkono lakini pia tulipitisha bajeti ya wizara ya Elimu ambapo serikali imeendelea kutenga bajeti kwa ajili ya kuwasaidia watoto wenye ulemavu na tutaendelea kupokea ili mazingira yawe rafiki kwa watoto wetu"Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Kasulu Ayubu Ngalaba Kilugu amemshukuru Profesa Ndalichako kwa moyo wa upendo na kujitoa kwa watoto wenye mahitaji maalumu huku akiomba msaada huo uendelee kufikishwa katika vituo vingine vyenye uhitaji.Naye Afisa Elimu Maalumu wa Halmashauri ya Mji Kasulu, Salvatory Kitogwe amesema Halmashauri ina shule tisa zinazohudumia watoto wenye mahitaji maalumu huku akisisitiza kuwa msaada huo utasaidia kuongeza ari ya wanafunzi katika masomo yao.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254








Post a Comment