" RC MHITA: WANANCHI JITOKEZENI KUPATA MSAADA WA KISHERIA BURE

RC MHITA: WANANCHI JITOKEZENI KUPATA MSAADA WA KISHERIA BURE

Na Mapuli Kitina Misalaba

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mboni Mhita, ametangaza kuanza kwa utekelezaji wa kampeni ya kitaifa ya Samia Legal Aid mkoani humo, itakayotoa huduma za msaada wa kisheria bure kwa wananchi kwa kipindi cha wiki mbili kuanzia Mei 6 hadi Mei 20, 2026.

Akizungumza na vyombo vya habari Mei 5, 2026, Mhita amesema kampeni hiyo inalenga kuwafikia wananchi wengi zaidi kwa kuwapeleka wataalamu wa sheria katika kata zote 130 za mkoa huo, ili kusaidia utatuzi wa migogoro na changamoto mbalimbali za kisheria zinazowakabili.

Ameeleza kuwa huu ni mwendelezo wa jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan za kuhakikisha haki inapatikana kwa urahisi, huku wananchi wakiepuka gharama za kufuata huduma za kisheria mbali na maeneo yao.

Ameongeza kuwa kampeni hiyo ni awamu ya pili kufanyika mkoani Shinyanga, ambapo katika awamu ya kwanza iliyotekelezwa mwaka 2023, jumla ya migogoro 578 ilishughulikiwa na kati yake 378 ilifanikiwa kutatuliwa, huku zaidi ya wananchi 22,000 wakinufaika na huduma hiyo.

Kwa mujibu wa Mhita, huduma zitakazotolewa katika kampeni hiyo ni pamoja na ushauri wa kisheria, utoaji wa elimu kwa umma kuhusu masuala ya sheria, uandaaji wa nyaraka mbalimbali za kisheria na uwakilishi katika vyombo vya utoaji haki.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Uzingatiwaji wa Msaada wa Kisheria, Osborn Paissi, amesema kampeni hiyo inalenga pia kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu haki zao na namna bora ya kuzilinda kupitia mifumo rasmi ya kisheria.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Kisheria Mkoa wa Shinyanga, John Shija, amesema wanatarajia mafanikio makubwa katika awamu hii ya pili, akibainisha kuwa huduma hizo zitawafikia wananchi wa makundi yote na kuchangia kupunguza migogoro katika jamii.

Ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki kampeni hiyo ili kunufaika na huduma hizo muhimu, ambazo zitaleta suluhisho la kudumu kwa changamoto za kisheria zinazowakabili.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post