" RC RUVUMA AKEMEA UDHALILISHAJI KWA WATUMISHI

RC RUVUMA AKEMEA UDHALILISHAJI KWA WATUMISHI

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Brigedia Jenerali Ahmed Abbas, amewataka viongozi wa taasisi za umma mkoani humo kuwatendea watumishi kwa heshima, utu na staha, huku akisisitiza changamoto zao zinapaswa kutatuliwa kwa busara badala ya lugha za matusi na vitendo vya kudhalilisha vinavyoshusha morali ya kazi.

Abbas ametoa kauli hiyo katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Mkoa wa Ruvuma yaliyofanyika Mei 9, 2026, akisema viongozi wanapaswa kutambua kuwa watumishi ni binadamu wenye familia zinazowategemea hivyo hawapaswi kubezwa wala kushushwa hadhi mbele za watu.

Amesema baadhi ya viongozi wamekuwa wakitumia lugha kali kwa watumishi jambo linaloathiri ufanisi wa kazi pamoja na mahusiano mahali pa kazi, huku akisisitiza kuwa uongozi bora unapaswa kujengwa katika misingi ya maadili, heshima na usikivu.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post