Ripoti ya Tume ya kuchunguza matukio ya baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025 imeweka bayana kuwa usalama wa taifa hauwezi kutegemea tu nguvu ya vyombo vya dola wakati wa machafuko, bali uwezo wa taasisi kutambua viashiria vya migogoro kabla havijalipuka.
Tume imebaini kuwa kabla ya Oktoba 26, kulikuwa na mijadala mikali mtandaoni iliyoashiria mipango ya kuhujumu miundombinu na vituo vya mafuta, lakini hatua stahiki hazikuchukuliwa kwa wakati.
Hili ni somo kwa mamlaka za mawasiliano na usalama kuwa taarifa za kiintelejensia zinapaswa kuleta majibu ya haraka ya kuzuia uhalifu badala ya kusubiri matukio yatokee.
Aidha, uchunguzi huo umebainisha kuwa utendaji usioridhisha wa baadhi ya watendaji wa umma katika ngazi za vijiji na kata ulichochea hasira miongoni mwa wananchi.
Pale kero za wananchi kama vile rushwa na ubadhirifu wa mali za umma zinapokosa majibu ya kuridhisha kwa muda mrefu, mazingira ya uvunjifu wa amani hujitengeneza yenyewe.
Ili kulinda utulivu wa nchi, ni lazima kuwepo kwa mfumo unaowajibisha watumishi wa umma na kuhakikisha kuwa malalamiko ya raia yanashughulikiwa kwa haki na uwazi, jambo ambalo litarejesha imani ya wananchi kwa serikali yao.
Hapa ndipo falsafa ya Mageuzi (Reforms) ya Rais Samia Suluhu Hassan inapopata umuhimu wake. Ili kuzuia marudio ya ghasia, ni lazima kufanya mageuzi makubwa katika mifumo ya kiutendaji, kuanzia ngazi za chini za serikali hadi taifa.
Wananchi wanahitaji kuona watumishi wa umma wanaowajibika na wanaosikiliza kero zao kwa wakati.
Taifa limebaini kuwa kuzuia vurugu kunahitaji serikali kuwa na uwezo wa kutambua mapema malalamiko ya wananchi kuhusu rushwa na ubadhirifu na kuyashughulikia kwa uwazi, jambo ambalo litaongeza Ustahimilivu (Resilience) wa taifa letu dhidi ya chokochoko zozote za kisiasa.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment