Na Mapuli Kitina Misalaba
Katika maadhimisho ya World Press Freedom Day, Mamlaka
ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) imetambua mchango mkubwa
wa vyombo vya habari katika kuhabarisha, kuelimisha na kuchochea maendeleo ya
jamii.
Akizungumza kwa niaba ya taasisi hiyo, Kaimu Mkuu wa
Kitengo cha Mawasiliano na Mahusiano kwa Umma wa SHUWASA Bwana Jonas Mush amesema
kuwa vyombo vya habari ni wadau muhimu ambao wamekuwa wakishirikiana kwa karibu
na mamlaka hiyo katika utekelezaji wa majukumu yake kwa muda mrefu.
Amesema kupitia vyombo vya habari, SHUWASA imekuwa
ikifikisha ujumbe kwa wananchi kwa urahisi zaidi, ikiwemo kutoa elimu kuhusu
huduma za maji na usafi wa mazingira pamoja na kuwahabarisha kuhusu shughuli
mbalimbali zinazotekelezwa na taasisi hiyo.
Aidha, ametoa wito kwa taasisi nyingine kuonyesha
ushirikiano kwa waandishi wa habari, hasa wanapohitaji taarifa au
wanapowasilisha changamoto za wananchi, ili kusaidia kuboresha utoaji wa huduma
kwa jamii.
Ameongeza kuwa uhuru wa vyombo vya habari ni kichocheo
cha maendeleo, akisisitiza kuwa taasisi zinazotoa nafasi kwa waandishi kufanya
kazi zao kwa uhuru hupata fursa ya kutambua na kutatua changamoto
zinazojitokeza kupitia taarifa zinazoripotiwa.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment