" THAMANI YA MAKAA YA MAWE YAFIKIA TRILIONI MOJA: TANZANIA KUWA KITOVU CHA NISHATI AFRIKA MASHARIKI NA KATI

THAMANI YA MAKAA YA MAWE YAFIKIA TRILIONI MOJA: TANZANIA KUWA KITOVU CHA NISHATI AFRIKA MASHARIKI NA KATI

 


Tanzania inaelekea kuwa kitovu cha uzalishaji wa nishati kupitia makaa ya mawe ambapo thamani ya madini hayo yaliyochimbwa imeongezeka kwa kasi kutoka shilingi bilioni 228.8 katika mwaka wa fedha 2020/21 hadi kufikia takribani shilingi trilioni moja mwaka 2022/23.

Uzalishaji umeongezeka kutoka tani 744,923 hadi kufikia tani 3,007,180 kwa mwaka, huku nchi ikiwa na akiba iliyothibitishwa ya takribani tani bilioni 5 katika mikoa ya Ruvuma, Songwe, Rukwa, na Njombe.

Kupitia msemaji wake Gerson Msigwa, Serikali imesema imejipanga kuboresha miundombinu ya barabara kuelekea migodini na kukuza soko la ndani ili makaa hayo yatumike zaidi katika kuzalisha vyuma, saruji, na nishati ya majumbani, hali itakayopunguza gharama za uzalishaji na kuongeza ushindani wa bidhaa za Tanzania katika masoko ya nje.

Wakati huo huo kuna mapinduzi mikubwa ya miundombinu katika mkoa wa Njombe. Imeelezwa katika mkutano na waandishi wa habari na msemaji wa serikali Geson Msigwa kuwa bajeti ya Tarura imeongezeka kwa asilimia 149 kwa lengo la kufungua barabara za mashambani.

Alisema Serikali ya Awamu ya Sita imeleta mageuzi makubwa ya miundombinu ya barabara mkoani Njombe kwa kuongeza bajeti ya TARURA kutoka wastani wa shilingi bilioni 8.44 hadi kufikia bilioni 21.07 kwa kipindi cha mwaka 2021-2026, ambalo ni ongezeko la asilimia 149.64.
AmesemaoOngezeko hilo limesaidia kuongeza mtandao wa barabara za lami kutoka kilometa 38.7 hadi kilometa 95.5, huku barabara za changarawe zikiongezeka na kufikia kilomita 2,097.40, jambo lililosaidia kufungua barabara mpya maeneo ya kilimo cha parachichi, chai, na viazi.

Aidha, ujenzi wa madaraja umeongezeka kutoka 352 hadi 386 na kalvati kufikia 2,962, hatua inayohakikisha kuwa asilimia 70 ya mtandao wa barabara mkoani humo unapitika katika majira yote ya mwaka, hivyo kurahisisha huduma za kijamii

Post a Comment

Previous Post Next Post