" UHAMIAJI SHINYANGA YAWARUDISHA WAHAMIAJI HARAMU 25, ONYO KALI LATOLWA

UHAMIAJI SHINYANGA YAWARUDISHA WAHAMIAJI HARAMU 25, ONYO KALI LATOLWA

Na Paul Kayanda, Shinyanga

Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Shinyanga imewarudisha zaidi ya wahamiaji haramu 25 kutoka nchini Burundi, Rwanda pamoja na nchi nyingine jirani, ikiwa ni sehemu ya oparesheni maalum ya kudhibiti uingiaji holela wa wageni nchini.

Akizungumza na vyombo vya habari Mei 25, 2026, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhamiaji Mkoa wa Shinyanga, Immanuel Kajula amesema wahamiaji hao wamekamatwa katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo kupitia oparesheni ya kawaida inayoendelea kufanyika.

Amesema baadhi ya raia hao wa Burundi walikamatwa katika migodi ya Mwakitolyo iliyopo wilayani Shinyanga Vijijini, ambapo walibainika kuingia nchini bila kufuata taratibu za kisheria.

“Wahamiaji hawa haramu wanasafirishwa kurejeshwa kwao kupitia mpaka wa Kabanga uliopo mpakani mwa Burundi na Rwanda,” amesema Kajula.

Aidha, afisa huyo amesema oparesheni hiyo ilianza rasmi Mei 25, 2026 na itaendelea kwa muda usiojulikana, huku akitoa onyo kali kwa watu wanaojihusisha na kuwaingiza wahamiaji nchini kinyume cha sheria.

“Hatutamvumilia mtu yeyote anayehusika kuwasafirisha au kuwahifadhi wahamiaji haramu. Sheria zitachukua mkondo wake,” alisisitiza.

Katika hatua nyingine, Kajula amesema Idara ya Uhamiaji imejipanga kuendelea kuimarisha ulinzi wa mipaka pamoja na kuwafikisha mahakamani watu wote watakaobainika kushiriki katika mtandao wa usafirishaji wa wahamiaji haramu kuingia Tanzania.


SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

 

Post a Comment

Previous Post Next Post