Vijana mkoani Ruvuma wamepatiwa mafunzo na kujengewa uzoefu kuhusu kilimo,lishe na masoko ,ili kuhakikisha vijana wanakua sehemu ya suluhisho la changamoto za ajira na maendeleo ya uchumi kwa kuongeza thamani ya mazao.Akifungua kikao hicho cha majadiliano kilichofanyika ukumbi wa Songea Chub Manispaa ya Songea Katibu Tawala mkoa wa Ruvuma Bi.Mary Makondo amesema sekta ya kilimo bado ndiyo mhimili mkuu wa uchumi mkoa Ruvuma,ambapo asilimia 85 ya wananchi wanategemea kilimo kwa maisha ya kila siku.Ameendelea kwa kupongeza jitihada zinazofanywa na GAIN za kuwajengea vijana uwezo wa uzalishaji,usindikaji na kuongeza thamani ya mazao kama hatua muhimu katika kujenga uchumi imara na jamii yenye afya bora pamoja na kupunguza hali duni ya lishe.Aidha, amewataka vijana kutumia jukwaa hilo kujifunza, kubadilishana uzoefu na kujenga mahusiano baina ya vijana na wadau mbalimbali wa maendeleo, taasisi za kifedha na masoko.Kwa upande wake mwakilishi wa shirika la GAIN Aileen Tinka lengo kuu la ni kuu la mafunzo ni kuwaunganisha vijana na masoko kutokana na fursa zilizopo mkoa wa Ruvuma zinazotokana na kilimo Ameendelea kuwa kupitia mradi wa ujasiriamali wa vijana kwa ajiri ya kesho ya chakula na kilimo (YEFFA) umeweza kuwafikia vijana 250 ambao wamepatiwa mafunzo tofauti tofauti ya uzalishaji mbegu,maharage lishe ,usalama wa chakula na kuongezaji thamani wa mazao Nao baadhi ya vijana wameeleza namna walivoweza kuboresha na kuinuka kimaisha baada ya kutambua fursa za kilimo kupitia mafunzo waliyopatiwa hapo awali
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


Post a Comment