Na Edington Mukiza Ezron, Misalaba Media
Baadhi ya wananchi katika Manispaa ya Shinyanga wamewataka vijana kuwajibika na kujishughulisha ili kuepukana na umasikini na kuliimarisha taifa kiuchumi.
Wameyasema hayo leo Mei,26,2026 kwa nyakati tofauti walipotembelewa
na Misalaba Media.
Akizungumza mmoja wa wananchi hao Dickson Christopher
amesema kuwa vijana wanatakiwa kupambana kujishughulisha na shughuli mbalimbali
za kiuchumi ili kujitengenezea maisha mazuri kwa sasa na badae kwani vijana
ndiyo nguzo ya jamii na taifa kwa ujumla.
Ameongeza kuwa vijana wanapofanya kazi za kuwaingizia
kipato husaidia katika kuimarisha uchumi wa jamii na wa taifa kwani huongeza
kiwango cha ulipaji Kodi hata uwekezaji nchini jambo ambalo linainua uchumi kwa
kiasi kikubwa.
Naye David John amesema kuwa baadhi ya vijana
wanashindwa kuwa wabunifu na kuwa na malengo jambo ambalo linawapelekea kukosa
kazi za kufanya na kufanya uharifu licha ya kuwepo fursa mbalimbali za
kiuchumi.
Pia amesema kuwa vijana wanatakiwa kupata mafunzo ya
ufundi na fani mbalimbali za kujiajiri kutokana na hali ya ukosefu wa ajira
kuliko kukaa mtaani bila kazi za kufanya ni muhimu wakawa na ujuzi juu ya fani
mbalimbali.
Wananchi hao wameendelea kusema kuwa vijana wanatakiwa
kuwa na maadili, nidhamu na kuepuka matendo yasiyofaa ili kuweza kufanikiwa
katika kazi zao wanazozifanya kwani nidhamu ndio misingi wa mafanikio.
Aidha wameiomba serikali kutoa fursa mbalimbali kwa
vijana ili kuwawezesha kiuchumi na kuboresha maisha yao na taifa ikiwemo kutoa
mikopo yenye riba nafuu na kutoa ajira kwa wingi katika kampuni na taasisi
mbalimbali.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment