" WACHIMBAJI WADOGO WA MGODI WA MWAKITOLYO NAMBA 6 WAIOMBA SERIKALI KUINGILIA MGOGORO WA LESENI

WACHIMBAJI WADOGO WA MGODI WA MWAKITOLYO NAMBA 6 WAIOMBA SERIKALI KUINGILIA MGOGORO WA LESENI

Wachimbaji wadogo wa dhahabu katika eneo la Mwakitolyo Namba 6, Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, wameiomba Serikali ngazi ya juu kuingilia kati mgogoro wa umiliki wa leseni unaoendelea katika eneo hilo.

Ombi hilo limetolewa katika kikao cha pamoja kilichowakutanisha wachimbaji hao, ambapo walieleza kuwa kwa muda mrefu wamekuwa wakifanya shughuli za uchimbaji katika eneo hilo na kulipa mirabaha ya Serikali bila kusumbuliwa.

Baadhi ya wachimbaji hao walisema wamekuwa wakitegemea shughuli hizo kama chanzo kikuu cha kipato, lakini kwa sasa wanakabiliwa na sintofahamu kufuatia kujitokeza kwa mtu anayedai kumiliki leseni ya eneo hilo.

Akizungumza na Misalaba Media, Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Kimadini Shinyanga, Mhandisi Noel Baraka ameeleza kuwa changamoto iliyopo ni kwamba mwenye leseni ameonekana hivi karibuni, hali iliyosababisha mvutano kati yake na wachimbaji waliokuwa tayari wanafanya kazi eneo hilo.

Amesisitiza kwamba kisheria mwenye haki ya eneo hilo ni mwenye leseni, lakini kutokana na mazingira yaliyopo, wachimbaji waliokuwapo awali hawawezi kuondolewa moja kwa moja bila kufuata taratibu ikiwemo makubaliano ya pamoja.

Kwa upande wao, wachimbaji wadogo wameeleza kushindwa kufikia mwafaka na mwenye leseni, hali iliyowalazimu kuiomba Serikali kupitia viongozi wa juu akiwemo Waziri wa Madini, Waziri Mkuu na Rais kuingilia kati mgogoro huo.

Wameeleza kuwa wamekuwa wakichimba katika eneo hilo kwa zaidi ya miaka 30, na walipoanza mchakato wa kufuatilia leseni walielezwa kuwa tayari kuna mtu anamiliki leseni ya eneo hilo, jambo ambalo linawashangaza kwani hawamfahamu na hajawahi kufanya shughuli zozote za uchimbaji katika eneo hilo.

Wachimbaji hao wameiomba Serikali iwape kipaumbele katika umiliki wa leseni hiyo ili waweze kuendelea na shughuli zao kwa amani na kuchangia maendeleo ya taifa.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post