Kikao cha Bodi ya Maji na wadau mbalimbali katika Halmashauri ya Mji Kasulu Mkoani Kigoma, kimependekeza bei mpya ya bili ya maji kwa lengo la kuboresha huduma hiyo na kumudu gharama za uendeshaji.Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Bongwe ambapo wadau wamependekeza kiwango kipya cha malipo kuwa kati ya shilingi 500 hadi 1,000 kwa unit moja ya maji.Akizungumza katika kikao hicho, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Kasulu Mjini (KUWASA) Samweli Kayombo, amesema mapendekezo hayo yatafanyiwa kazi kwa lengo la kutatua changamoto za miundombinu ya maji katika eneo hilo.Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Sabinus L. Chaula amesema ni muhimu kufanya tathmini kubaini wateja wanaotumia na wasiotumia mita sambamba na kuhakikisha mita zinapatikana.Aidha, Kaimu Mkurugenzi amewataka watumishi wa huduma ya maji kufanya kazi kwa uaminifu na uwajibikaji ili kuondoa kero kwa wananchi.Akifunga kikao hicho, Katibu Tawala wa Wilaya ya Kasulu Theresia Mtelewe amewasisitiza viongozi wa serikali za mitaa kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu mabadiliko ya bei ya maji pamoja na kusimamia miundombinu yote ili huduma hiyo iwe endelevu.SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
















Post a Comment