" WAKUU WA IDARA NA VITENGO TUNDURU WAJENGEWA UWEZO MATUMIZI YA MFUMO WA IFT-MIS KUIMARISHA USIMAMIZI WA FEDHA

WAKUU WA IDARA NA VITENGO TUNDURU WAJENGEWA UWEZO MATUMIZI YA MFUMO WA IFT-MIS KUIMARISHA USIMAMIZI WA FEDHA


Wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru wamepewa mafunzo maalumu kuhusu matumizi ya Mfumo wa Ukaguzi na Usimamizi wa Fedha katika Mamlaka za Serikali za Mitaa (Inspection and Financial  Tracking Management Information System - IFT-MIS), kwa lengo la kuimarisha uwajibikaji na usimamizi wa rasilimali za umma.Mafunzo hayo yamefanyika  katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru lengo ni kuhakikisha usimamizi wa fedha unazingatia taratibu, sheria na mifumo ya kisasa ya kidijitali iliyowekwa na Serikali.Akiongoza mafunzo hayo, Mkufunzi ambaye pia ni Katibu Tawala Msaidizi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Bwan. Piniel Mbura, amesema kuwa mfumo wa IFT-MIS ni chombo muhimu kinacholenga kuleta mapinduzi katika sekta ya ukaguzi wa ndani na usimamizi wa fedha ndani ya Mamlaka za Serikali za Mitaa.Lengo kuu la Serikali ni kuhakikisha kuwa kila idara inakuwa na uelewa mpana wa mfumo huu. IFT-MIS inasaidia kurahisisha ufuatiliaji wa matumizi ya fedha, kuripoti vihatarishi, na kuhakikisha hoja za ukaguzi zinashughulikiwa kwa wakati na kwa usahihi kabla ya ukaguzi wa nje.Katika mafunzo hayo, washiriki wameelekezwa namna mfumo huo unavyofanya kazi, ikiwa ni pamoja na: Kuongeza uwazi katika mchakato mzima wa ukaguzi wa ndani, Kupunguza matumizi ya makaratasi na kuongeza kasi ya upatikanaji wa taarifa za kifedha, Kuimarisha mifumo ya udhibiti wa ndani ili kuzuia mianya ya upotevu wa mapato ya Serikali, Aidha, imeelezwa kuwa kupitia mfumo huu, Wakuu wa Idara na Vitengo wataweza kuona na kufanyia kazi hoja zinazowahusu moja kwa moja kwenye maeneo yao ya utendaji, jambo litakalopelekea Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru kuendelea kupata hati Safi katika ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).Mafunzo haya ni mwendelezo wa jitihada za Serikali katika kuimarisha mifumo ya TEHAMA ili kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi na kuhakikisha thamani ya fedha (Value for Money) inaonekana.



SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

 

Post a Comment

Previous Post Next Post