Na Eunice Kanumba – Shinyanga.
Serikali kupitia wizara ya afya inatarajia kuendesha zoezi la utoaji wa chanjo ya matone ya polio kuanzia Mei 7-10, 2026 kwa watoto chini ya miaka kumi ikiwa ni awamu ya pili baada ya awamu ya kwanza kutolewa kwa watoto wa umri huo Machi 2026.
Katika kujenga uelewa wa pamoja juu ya chanjo hiyo, ili kuwafikia walengwa serikali leo tarehe 4 maya 2026 imeendesha mafunzo kwa wadau wenye ushawishi kutoka katika jamii, ili zoezi hilo la chanjo kwa awamu ya pili liweze kutekelezeka kwa ufasaha.

Akizungumza wakati akiwasilisha mada juu ya ugonjwa wa polio na chanjo hiyo Mratibu wa Chanjo Manispaa ya Shinyanga, Ramadhani Maneno amesema lengo la mafunzo hayo ni kujengeana uelewa wa pamoja juu ya nini kinachokwenda kufanywa na serikali katika zoezi la kitaifa linalojumuisha mikoa ya Shinyanga,Geita Mara Singida Simiyu Kagera na Tabora.
Amesema kwa upande wa manispaa ya Shinyanga Jumla ya watoto 71,966 wanaoanzia umri wa miaka kumi kushuka chini wanatarajiwa kupatiwa chanjo kwa amu ya pili ili kuwajengea kinga Zaidi juu ya ugonjwa huo hatari unaopelekea mtoto kupooza na kupata ulemavu wa ghafla.

Maneno ameanisha kuwa katika kutekeleza jukumu hilo kwa weledi Manispaa ya Shinyanga tayari imeandaa timu 91 zitakazohudumia jamii ambapo timu 83 zitatembea nyumba kwa nyumba kutoa huduma za chanjo hiyo huku timu 8 zikipita katika maeneo maalum kama vile katika masoko na maeneo ili kuhakikisha hakuna mtoto mwenye umri chini ya miaka kumi anakosa chanjo hiyo kwa ustawi wa jamii imara.
Kwa upande wake Mwakilishi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI idara ya afya, Linda Chatila amesema chanjo hiyo sio jambo jipya ilikuwa ikitolewa hata siku za nyuma lakini kwa sasa inatolewa kwa kampeni maalum kufuatia kugundulika vimelea vya ugonjwa huo katika maji taka jijini Mwanza hali iyopelekea serikali kuchukua hatua za maksudi ilikuinusru jamii na ugoonjwa huo.

“Polio haina tiba, lakini inazuilika kwa chanjo. Ni muhimu wazazi kuhakikisha watoto wao wanapata chanjo hii kwa wakati,” amesema Chatila
Amesisitiza kuwa chanjo hiyo ni salama kwa watoto wote walio chini ya miaka 10, na kuonya kuwa mtoto atakayekosa chanjo atakuwa kwenye hatari kubwa ya kupata ugonjwa huo huku akiwasihi wazazi kuachana na uvumi potofu juu ya chanjo hiyo kwamba ina madahra kwa watoto na kuanisha kuwa chanjo hiyo ni salama na imethibitishwa na shirika la afya duniani (WHO), pamoja na wizara ya afya na masuala ya vifaa ya tiba (TMDA).

Nao baadhi ya wadau walioudhuria mafunzo hayo akiwemo, Kamanda Mkuu wa Sungusungu Mkoa wa Shinyanga, John Kadama amesema kuwa ameipongeza serikali kwa uamuzi huo wa kuwanusuru watoto dhidi ya ugonjwa huo na kwamba jeshi la sungusungu litatoa ushrikiano ili kuhakikisha zoezi hilo linafanyika ipasavyo.
Awali, Mwenyekiti wa Baraza la ushauri la Wazee Manispaa ya Shinyanga, Stephano Tano amewaasa wazazi na walezi kuhakikisha watoto walio chini ya umri wa miaka kumi wanapatiwa chanjo hiyo, ili kuzuia lemavu na vifo kwa watoto.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
Post a Comment