" MEYA JIJINI ARUSHA AWAPONGEZA TAKUKURU

MEYA JIJINI ARUSHA AWAPONGEZA TAKUKURU

*Abainisha mikakati iliyowekwa kuhakikisha Jiji la Arusha kuwa na miundombinu imara*Na, EGIDIA VEDASTO, Misalaba Media, Arusha.Mstahiki Meya wa Halmashaurinya Jiji la Arusha Maxmillian Iranqhe ametoa pongezi Kwa ofisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU waliofanikiwa kuwanasa watumishi wawikibwa halmashauri  hiyo waliobainika kutafuna fedha za miradi ya maendeleo.Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake wakati akiwasilisha miradi iliyosainiwa na  inayoenda  kutekelezwa kuanzia robo ya kwanza hadi ya nne ya mwaka 2025/2026  amesema watumishi wasio waaminifu ni kikwazo cha maendeleo na hawastahili kufumbiwa macho.Aidha ametaja miradi inayoenda kutekelezwa kuwa ni pamoja na ujenzi wa barabara za ndani Kwa kiwango cha zege, matengenezo ya boksi calvati na mitaro Kwa gharama ya jumla  shilingi Billions 3.72 zilizotokana na mapato ya ndani ya halmashauri ya Jiji la Arusha."Ninawaahidi wananchi kuwa maendeleo haya yatafika kila sehemu na kila mmoja atashuhudia katika eneo lake, niwakumbushe Waheshimiwa Madiwani waendelee kuwaeleza wananchi juu ya miradi hii mikubwa inayotekelezwa na Serikali awamu ya sita"Hatahivyo Maxmillian amesema miradi hiyo itakamilika ndani ya kipindi cha miezi sita, na mkandarasi atakayechelewesha mradi hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.Sambamba na hayo amesisitiza wananchi kutunza mazingira Kwa kufanya usafi na kuwataka waliosaini mikataba ya kusimamia usafi wa Jiji kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao sawa na taratibu zinavyowataka.Maxmillian amesema kuwa ujenzi wa barabara Kwa kiwango cha zege utakuwa chini ya Mkandarasi JIANGXI GEO ENGINEERING GROUP COOPERATION LTD, na Wakandarasi wengine watakaojenga maboksi cavati na mitaro ni  pamoja na M/s Raz Builders(T)Limited, M/s ZOWANGE JR ENTERPRISES LIMITED na M/s MANDAKA (T) LIMITED.

 SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post