" AJALI: GARI LA MAFUTA LATEKETEA KWA MOTO TUNDURU, DEREVA AFARIKI DUNIA

AJALI: GARI LA MAFUTA LATEKETEA KWA MOTO TUNDURU, DEREVA AFARIKI DUNIA

Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma limetoa ufafanuzi kuhusu ajali ya gari lililokuwa limebeba mafuta kutoka Mkoa wa Mtwara kuelekea nchini Zambia, ambalo liliacha njia na kuwaka moto katika Kijiji cha Huria, Kata ya Matemanga, Tarafa ya Matemanga, Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma.

Akitoa taarifa ya ajali hiyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, SACP Marco Chilya, amesema kuwa mnamo tarehe 2 Juni 2026 majira ya saa 4:00 asubuhi, katika Kijiji cha Huria, Kata ya Matemanga, Tarafa ya Matemanga, Wilaya ya Tunduru, kwenye barabara kuu ya Tunduru–Songea, gari lenye namba za usajili T 833 EFY aina ya TATA NOVUS Tank la mafuta, mali ya kampuni ya SOUND INDUSTRY LTD ya Dar es Salaam, likiendeshwa na dereva aliyetambulika kwa jina la Adam Abraham (46), mkazi wa Boko-Bunju jijini Dar es Salaam, likiwa limebeba mafuta ya petroli kutoka Mtwara kuelekea Zambia, liliacha njia, kupinduka na baadaye kuwaka moto.

Kamanda Chilya amesema ajali hiyo ilisababisha kifo cha dereva wa gari hilo, huku moto ulioteketeza gari hilo ukisababisha upotevu mkubwa wa mafuta yaliyokuwa yamebebwa.

Aidha, amesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi uliomfanya dereva kushindwa kulimudu gari lake alipofika kwenye kona. Ameongeza kuwa mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Tunduru kwa ajili ya taratibu nyingine.

Kamanda Chilya ametoa wito kwa madereva na wamiliki wa vyombo vya moto kuwa waangalifu wanapovitumia, kufuata sheria na kanuni za usalama barabarani, pamoja na kuepuka mwendo kasi ili kupunguza ajali zisizo za lazima.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post