" ALLY HAPI ALIVYOWAPIGA 'MSASA' CHADEMA

ALLY HAPI ALIVYOWAPIGA 'MSASA' CHADEMA

 

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi Tanzania wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ally Salum Hapi, amepokelewa mkoani Shinyanga ambapo katika mkutano wake wa hadhara amewataka viongozi na wanachama wa CHADEMA kuelekeza nguvu zao katika kuwasilisha hoja za maendeleo badala ya kuendelea na malalamiko ya kisiasa.


Hapi amesema kuwa baada ya baadhi ya viongozi wa chama hicho kutoka kifungoni na kuanza tena mikutano ya kisiasa, wananchi walitarajia kusikia sera na mikakati ya kuboresha maisha yao, lakini badala yake wameendelea kusikia lawama na malalamiko yasiyoleta suluhisho la changamoto za wananchi.

Amesisitiza kuwa ushindani wa kisiasa unapaswa kujengwa kwenye hoja, sera na mipango ya maendeleo inayoweza kuinua uchumi, kuongeza ajira na kuboresha huduma za jamii.

Aidha, amewataka wananchi wa Shinyanga kuendelea kuiunga mkono Serikali ya CCM chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan kwa mafanikio yanayoendelea kupatikana katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo nchini.

Post a Comment

Previous Post Next Post