Chama Cha Waajiri (ATE) , Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) waingia makubaliano ya ushirikiano wa kimkakati ili kuimarisha mifumo ya hifadhi na ajira nchini.TUCTA yatoa wito wa ushirikishwaji na ruksa ya wafanyakazi kujiunga vyama ya wafanyakazi Na Damas Makangale , Dar es Salaam Ushirikiano wa kimkakati kati ya Chama Cha Waajiri na Mfuko wa Hifadhi wa Jamii (NSSF) ni makubaliano yenye kufungua fursa ya kujenga mazingira ya kuboresha usalama na kinga ya kijamii cha waajiri na wafanyakazi kwenye sekta ya umma na binafsi na kuchochea ukuaji wa biashara na uchumi wa nchini kwa ujumla.Akizungumza kwenye mkutano mkuu wa 67 wa wanachama na kongamano la waajiri nchini, Waziri wa Nchini , Ofisi ya Waziri Mkuu , Kazi , Ajira na Mahusiano , Deus Sangu amesema kwamba makubaliano ya hayo ni fursa ya kujenga uelewa wa pamoja kati ya mifuko na chama cha waajiri na kupanua wigo wa kuwahudumia wafanyakazi na waajiri kwa ufanisi zaidi.“Serikali ya awamu ya sita sikivu nilisikia kilio cha waajiri nchini kuhusu tozo na malimbikizo ya michango ya wafanyakazi na kuiagiza Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kuoandoa tozo kwa waajiri hasa wale waliokuwa na malimbikizo ya michango ya wafanyakazi,” “Na hatua hii itasaidia kwa kiasi kikubwa kuelekeza fedha hizo kwenye kupanua wigo wa biashara zetu na mitaji na uwekezaji ili kuongeza tija kwenye uzalishaji mali na kuchochea uchumi wa nchini kwa kulipa kodi mbalimbali,” amesema Sangu Waziri Sangu alitumia fursa hiyo kuwakumbusha waajiri nchini kutekelezwa takwa la kisheria la serikalila kima cha chini cha mshahara na kuendelea kuheshimu sheria za nchini kwa kusaini mikataba bora ili kuweka mazingira ya amani na wafanyakazi mahali pa kazi.Aliongeza kwamba ni muhimu kwa waajiri nchini kuendelea kuboresha mazingira ya kazi na kulinda haki kifadhi za jamii wa watumishi wake ikienda pamoja na kutafakari kesho yao baada ya kustaafu.“Mkaubaliano ya leo kati ya ATE NA NSSF ya maslahi mapana kwa wafanyakazi nchini kwenye sekta iliyo rasmi na isiyo rasmi kwa kuangalia na kutizama kwa kina kesho ya wafanyakazi pindi watapostaafu kazi aweze kumudu gharama za maisha kwa michango aliyojiwekea.Kwa upande wake , Afisa Mtendaji Mkuu wa Chama Cha Waajiri nchini (ATE) . BI. Suzanne Ndomba Doran amesema kwamba kongamano hilo linatoa nafasi ya kujadiliana , kujenga uelewa wa pamoja na kukubaliana hatua zinazoweza kutekelezeka.Aliongeza kwamba mfumo bora wa hifadhi ya jamii lazima ujenge uwiano kati ya ulinzi wa mafanyakazi na uwezo wa biashara kuendelea kukua na kuchangia Pato la Taifa kwa ujumla.” Kauli mbiu hii inalenga kuimarisha hifadhi ya jamii na uendelevu wa biashara kupitia ushirikiano wa kimkakati, ufanisi wa kanuni na uhsirikiano wa taasisi.“ Kauli mbiu hii inatukumbusha jambo moja la msingi: ustawi wa mfanyakazi na uhai wa biashara ni mambo yanayokwenda pamoja,” amesema Bi Ndomba. Aliongeza kwamba waajiri wanaunga mkono hifadhi ya jamii kwa sababu mfanyakazi mwenye usalama wa kijamii hupata utulivu na kuongeza tija mahali pa kazi na kusukuma mbele maendeleo endelevu ya taasisi na nchini kwa ujumla.Bi Ndomba alifafanua kwamba maeneo matatu yanapaswa kupewa kipaumbele katika mfumo wa kazi na ajira nchini kwanza kuimarisha ushirikiano wa kimkakati kati ya waajiri na taasisi za hifadhi ya jamii ili kuongeza ufanisi wa kanuni na taratibu ili kupunguza urudufu , ucheleweshaji wa huduma na gharama zisizo za lazima.Alifafanua kwamba pamoja na mambo mengine ushirikiano kwa kimkakati itajenge mshikamano wa taasisi unaowezesha kubadilishana taarifa, kutumia mifumo ya kidijitali na kutoa huduma kwa wakati. Kwa upande wake , katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Hery Mkunda amesema kwamba kwa upande wa wafanyakazi wanaamini kwamba mifumo ya kinga ya jamii ikiimaishwa itasaidia wafanyakazi kuboresha kipato chao na kuimarisha usalama wa afya zao mahali pa kazi.“Niseme tu nimefurahishwa na Mada kuu ya Majadiliano katika Mkutano wa mwaka huu ambayo inasema “Kuimarisha Kinga ya Jamii na Uendelevu wa Biashara kupitia Ushirikiano wa Kimkakati, Kurahisisha Taratibu za Udhibiti, na Kuunganisha Mifumo ya Taasisi”“Mada hii ni muhimu kwetu sote kwani inasisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya Serikali, Vyama vya Wafanyakazi, Waajiri, Taasisi za hifadhi ya jamii na washirika wa maendeleo katika kujenga mazingira wezeshi kwa ukuaji shirikishi wa uchumi,” amesema Mkunda Mkunda alitoa wito kwa waajiri wite nchini kuimarisha dhana ya ushirikishwaji katika maeneo yao ya kazi kwa kuwashirikisha wafanyakazi (Vyama vya Wafanyakazi) pamoja na kutoa uhuru kwa watumishi kujiunga na vyama vya wafanyakazi.Naye Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) , Masha Msomba amesema makubaliano yaliyotiwa saini ya ushirikiano kati ya NSSF na ATE ni ushahidi tosha ya kwamba kuna umuhimu wa kuimarisha mifumo ya hifadhi na vyama vya waajiri na wafanyakazi hapa nchini.“Ushirikiano huu utakuza ajira zenye staha na kuimarisha mifumo ya ajira na michango ya wafanyakazi na kusukuma mbele maendeleo ya biashara na uwekezaji wenye tija wa sekta binafsi hapa nchini.Aliongeza kwamba Dira ya Taifa 2050 inataka tujipange na kupanua wigo wa huduma ya hifadhi ya jamii kwenye sekta binafsi na ajira zilizo na zisizo rasmi nchini ili kuleta chachu ya ukuaji wa sekta binafsi katika kutoa ajira na mchango kwa ukuaji wa uchumi wa nchini.
Waziri wa Nchini , Ofisi ya Waziri Mkuu , Kazi , Ajira na Mahusiano , Deus Sangu akizungumza kwenye mkutano mkuu wa 67 wa wanachama na kongamano la waajiri nchini lililoandaliwa na Chama cha Waajiri nchini (ATE)
Waziri wa Nchini , Ofisi ya Waziri Mkuu , Kazi , Ajira na Mahusiano , Deus Sangu akizungumza kwenye mkutano mkuu wa 67 wa wanachama na kongamano la waajiri nchini lililoandaliwa na Chama cha Waajiri nchini (ATE)
Afisa Mtendaji Mkuu wa Chama Cha Waajiri nchini (ATE) . BI. Suzanne Ndomba Doran akizungumza na waajiri na wageni waalikwa katika mkutano wa 67 wa wanachama na kongamano la waajiri nchini
Waziri wa Nchini , Ofisi ya Waziri Mkuu , Kazi , Ajira na Mahusiano , Deus Sangu akisalimiana na katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Hery Mkunda
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) , Masha Msomba (kushoto aliyekaa) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Chama Cha Waajiri (ATE) Bi Suzanne Ndomba Doran (Kulia aliyekaa) wakitia saini makubaliano hayo ya ushirikiano (Memorandum of Understanding -MOU)
Mkuruggenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Masha Msomba na Afisa Mtendaji Mkuu wa Chama Cha Waajiri (ATE) wakibadilishana hati za makubaliano SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment