Katibu Tawala wa Wilaya ya Kasulu, Theresia Mtewele amewahimiza wanawake kutumia nishati safi ikiwemo majiko banifu, mkaa mbadala, gesi na umeme kama sehemu ya juhudi za kutunza mazingira na kukabiliana na uharibifu wa mazingira.Ameyasema hayo wakati wa maadhimisho ya siku ya Mazingira yaliyofanyika katika Halmashauri ya Mji Kasulu sambamba na utambulisho wa taasisi isiyo ya kiserikali ya Tanzania Women Empowerment Network (TAWEN) inayojihusisha na kuwawezesha wanawake kiuchumi na kijamii.Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kasulu amewataka wanawake kuepuka mikopo isiyofuata taratibu na yenye riba kubwa huku akiwahimiza kutumia fursa mbalimbali za kiuchumi zinazopatikana kupitia taasisi rasmi za kifedha.Maadhimisho hayo yamefanyika kwa namna ya kipekee kupitia jukwaa maalumu la wanawake ambapo washiriki wamepata fursa ya kujadili masuala mbalimbali muhimu ikiwemo matumizi ya nishati safi, fursa za kiuchumi zinazopatikana Kasulu na Mkoa wa Kigoma kwa ujumla pamoja na huduma zinazotolewa na taasisi za serikali na binafsi zikiwemo TANESCO, NSSF na benk NMB.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254






















Post a Comment