Na Mapuli Kitina Misalaba
Baada ya ushindi wa mchezo wa kwanza, timu ya Nyandolwa
FC imeendelea kuonesha ubabe wake katika mashindano ya NIACHEKONA CUP 2026
baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Bajaji FC derby katika mchezo wa
marudiano uliochezwa leo Juni 2, 2026 katika uwanja wa Mwabenda, Kata ya Solwa,
Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.
Ushindi huo unaifanya Nyandolwa FC kufuzu hatua
inayofuata ya mashindano hayo kwa jumla ya mabao 2-0, baada ya kushinda mchezo
wa kwanza kwa bao 1-0 dhidi ya wapinzani wao Bajaji FC.
Kwa ushindi huo, Nyandolwa FC sasa itasubiri mshindi
wa mchezo wa kesho ili kufahamu mpinzani wake katika hatua inayofuata ya
NIACHEKONA CUP 2026.
Akizungumza baada ya mchezo huo, Katibu wa Mashindano
hayo ametangaza kuwa mchezo unaofuata utachezwa kesho ambapo Lyabukande FC
itamenyana na Shilabela FC katika pambano linalotarajiwa kuwa na
ushindani mkubwa.
Ameendelea kuwakaribisha wananchi wa Solwa na maeneo
jirani kujitokeza kwa wingi katika uwanja wa Mwabenda ili kushuhudia vipaji vya
vijana na burudani ya soka kupitia mashindano hayo.
Mashindano ya NIACHEKONA CUP 2026 yameandaliwa na mdau
wa michezo Paul Daud Augustino maarufu MC NIACHEKONA kwa ufadhili wa shirika
la Lushu Foundation ikiwa lengo ni kuibua vipaji vya vijana, kuimarisha amani
na kuendeleza michezo katika jamii.
Kwa huduma za ushereheshaji wa shughuli mbalimbali, matangazo na matukio ya kijamii, MC NIACHEKONA anapatikana kupitia namba 0757 267 738.
"NIACHEKONA CUP MWABENDA – WEKA TU
WEKE."
Wachezaji wa NYANDOLWA FC na BAJAJI FC wakioneshana uwezo mkubwa katika Derby ya Wachimbaji iliyochezwa katika uwanja wa Mwabenda leo Juni 2, 2026.
Wachezaji wa NYANDOLWA FC na BAJAJI FC wakioneshana uwezo mkubwa katika Derby ya Wachimbaji iliyochezwa katika uwanja wa Mwabenda leo Juni 2, 2026.
Mchezo ukiendelea huku timu zote zikisaka ushindi muhimu wa kusonga mbele katika mashindano ya NIACHEKONA CUP 2026.
Viongozi wa mashindano na wadau wa michezo wakifuatilia kwa karibu mchezo wa NYANDOLWA FC dhidi ya BAJAJI FC.
Viongozi wa mashindano na wadau wa michezo wakifuatilia kwa karibu mchezo wa NYANDOLWA FC dhidi ya BAJAJI FC.
Watangazaji wa mechi.
Sehemu ya wananchi waliojitokeza kushuhudia burudani ya soka kupitia mashindano ya NIACHEKONA CUP 2026.
Sehemu ya wananchi waliojitokeza kushuhudia burudani ya soka kupitia mashindano ya NIACHEKONA CUP 2026.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254














Post a Comment