" IVORY COAST YATINGA HATUA YA 32 BORA KWA KUICHAPA CURACAO 2-0

IVORY COAST YATINGA HATUA YA 32 BORA KWA KUICHAPA CURACAO 2-0

 


Mshambuliaji Nicolas Pepe aliiongoza Ivory Coast kutinga hatua ya 32 bora ya Fainali za Kombe la Dunia 2026 baada ya kufunga mabao mawili katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Curacao.

Pepe alianza kuifungia Ivory Coast mapema katika dakika ya saba, akimalizia kwa mguu wa kushoto krosi ya winga Yan Diomande.
Baada ya bao hilo, pande zote mbili zilicheza kwa kasi na kutengeneza nafasi kadhaa, lakini zilikosa umakini wa kuzitumia. Hivyo, kipindi cha kwanza kilimalizika Ivory Coast ikiwa mbele kwa bao 1-0.

Kipindi cha pili kilianza kwa Curacao kushambulia kwa lengo la kusawazisha, lakini ilishindwa kutumia nafasi ilizopata. Kipa wa Ivory Coast, Issa Fofana, alifanya kazi kubwa kwa kuokoa mashambulizi mawili hatari na kuendelea kuilinda timu yake.

Pepe alikamilisha ushindi huo kwa kufunga bao la pili dakika ya 64, akimalizia pasi ya Ibrahim Sangare.

Matokeo hayo yameirejesha Ivory Coast kwenye mstari wa ushindi baada ya kupoteza mechi iliyopita kwa mabao 2-1 dhidi ya Ujerumani.

Kwa ushindi huo, Ivory Coast imefikisha pointi sita na kumaliza katika nafasi ya pili ya Kundi E, ikiwa na idadi sawa ya pointi na vinara Ujerumani. Wajerumani walimaliza kileleni licha ya kufungwa mabao 2-1 na Ecuador.

Ecuador, iliyofikisha pointi nne, pia imefuzu hatua ya 32 bora kupitia nafasi ya timu nane bora zilizomaliza katika nafasi ya tatu kwenye makundi yao (Best Losers). Curacao ilimaliza mkiani mwa kundi ikiwa na pointi moja.

Ivory Coast imeandika historia kwa kufuzu hatua ya 32 bora kwa mara ya kwanza, baada ya kushindwa kufanya hivyo katika majaribio yake matatu yaliyopita. Sasa imeungana na Morocco na Afrika Kusini, ambazo tayari zilikuwa zimekata tiketi ya hatua hiyo.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post