" KAMPENI YA MAADILI NA NALEZI CHANYA YATEKELEZWA ARUSHA

KAMPENI YA MAADILI NA NALEZI CHANYA YATEKELEZWA ARUSHA

Na, Egidia Vedasto,

Misalaba Media,Arusha.

Mkoa wa Arusha umeanza kutekeleza maelekezo rasmi ya kuendesha kampeni ya maadili na malezi chanya kwa jamii, kampeni hiyo inalenga kuhamasisha wazazi, walezi na jamii kwa ujumla kuhusu umuhimu wa malezi bora kwa watoto.

Akizungumza na Mwandishi wa habari wa chombo hiki ofisini kwake Afisa ustawi wa jamii mkoa wa Arusha Dennis Mgiye amesema hatua hiyo inaenzi maazimio mbalimbali ya kimataifa kuhusu haki na ustawi wa mtoto wa Afrika. Moja ya maazimio hayo ni Azimio la Umoja wa Afrika la mwaka 1991 lililolenga kulinda haki za watoto barani Afrika.

"Historia ya Siku ya Mtoto wa Afrika ilianzia nchini South Africa mwaka 1976. Wanafunzi wengi waliuawa wakati wakidai haki yao ya kupata elimu bila ubaguzi wa aina yoyote.

Kutokana na historia hiyo, serikali imeendelea kuweka mikakati ya kuhakikisha watoto wanapata malezi bora na elimu sahihi ya maadili.Juhudi hizo zinalenga kujenga kizazi chenye heshima na uwajibikaji"amesema.

Ameongeza kuwa Wizara ya maendeleo ya jamii, jinsia wanawake na makundi Maalum kwa kushirikiana na Wizara ya habari, sanaa michezo na utamaduni wamezindua mwongozo wa kitaifa wa masuala ya maadili. Mwongozo huo unatarajiwa kusaidia utoaji wa elimu kwa jamii katika maeneo mbalimbali nchini.

Aidha, amebainisha kuwa mkoa wa Arusha ni miongoni mwa mikoa iliyopewa jukumu  la kutekeleza kampeni ya  utoaji wa elimu ya maadili na malezi chanya ambapo kwa mwezi wote wa Juni,

Elimu hiyo itawafikia watoto, wazazi pamoja na walezi kupitia mikutano na kampeni maalum.

Vilevile Wakurugenzi wa halmashauri, wakuu wa wilaya pamoja na maafisa ustawi wa jamii wamepewa jukumu la kuhakikisha elimu hiyo inawafikia wananchi. watahamasisha jamii kushiriki katika malezi na makuzi bora ya watoto.

Kwa upande mwingine, Ofisi ya Afisa ustawi wa jamii mkoa Kwa kushirikiana na  wadau wa malezi ya watoto wanatarajia kushirikiana kufanya tamasha kubwa katika Shule ya Sekondari Arusha. Lengo kuu ni kuona jamii inabadilika, inaelimika na kujenga taifa lenye watu wenye maadili mema.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post