" KATAMBI: AMANI NA USALAMA NI KIPAUMBELE CHA SERIKALI

KATAMBI: AMANI NA USALAMA NI KIPAUMBELE CHA SERIKALI

 

Serikali ya Tanzania imeahidi kuendelea kulinda, kusimamia na kutekeleza haki za binadamu ikiwemo haki za raia wa Tanzania pamoja na wakimbizi kutoka mataifa mbalimbali wanaohifadhiwa nchini.

Akizungumza na wakimbizi wanaoishi jijini Dar es Salaam waliowawakilisha wenzao kutoka maeneo mbalimbali nchini, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi amesema Serikali itaendelea kuhakikisha amani na usalama wa nchi unadumishwa ili madhira yanayotokea katika mataifa mengine yasitokee Tanzania.

Katambi amesema Tanzania imekuwa mfano wa kuigwa katika ukarimu kwa wakimbizi, lakini pia imejifunza kutokana na hali ya usalama inayojitokeza katika nchi jirani, hivyo inaimarisha mifumo yake ya ulinzi na usimamizi.

Ameongeza kuwa Serikali itaendelea kuwahudumia wakimbizi kwa kuzingatia misingi ya haki za binadamu, sheria za nchi pamoja na mikataba ya kimataifa inayosimamia masuala ya wakimbizi.

Aidha, amesisitiza kuwa usalama wa nchi utaendelea kuwa kipaumbele cha Serikali huku akiwataka wakazi na wakimbizi kushirikiana katika kudumisha amani na mshikamano wa kijamii.

 SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post