Na Mapuli Kitina Misalaba
Macho na masikio ya mashabiki wa soka leo yataelekezwa
katika Uwanja wa Mwabenda, Kata ya Solwa, ambapo mabingwa watetezi wa NIACHEKONA
CUP, Sangu FC kutoka Wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza, watashuka dimbani
kumenyana na Bulige FC kutoka Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga katika mchezo
unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.
Sangu FC wanaingia katika mchezo huo wakiwa na dhamira
ya kuendelea kutetea ubingwa wao walioutwaa katika msimu wa 2024/2025, huku
Bulige FC nao wakisaka ushindi utakaowaweka katika nafasi nzuri ya kusonga
mbele kwenye mashindano hayo.
Pambano hilo linafunga rasmi hatua ya kwanza ya
mzunguko wa pili wa mtoano wa NIACHEKONA CUP 2026, hatua iliyoshuhudia timu
mbalimbali zikipambana kusaka nafasi ya kuingia katika kundi la timu 12 bora za
mashindano hayo.
Mashabiki wengi wamekuwa wakijiuliza kama Sangu FC
wataendelea kuonyesha makali yao na kuthibitisha ubora wao kama mabingwa
watetezi au kama Bulige FC wataweza kuandika historia kwa kuwazuia kuendelea na
safari ya kutetea ubingwa.
Baada ya mchezo wa leo, kuanzia Jumapili Juni 7, 2026,
mashindano yataingia rasmi katika hatua ya timu 12 bora, ambapo mfumo wa
mashindano utakuwa wa mtoano wa moja kwa moja (Knockout).
Katika hatua hiyo, timu zitakapokutana mshindi
ataendelea na mashindano huku timu itakayofungwa ikiondolewa moja kwa moja,
hali inayotarajiwa kuongeza ushindani na presha kwa kila timu.
Baadhi ya michezo iliyopangwa kuchezwa katika hatua ya
timu 12 bora ni pamoja na:
Nyundo FC dhidi ya
Mawemiru FC, Duara FC dhidi ya Songambele Mhangu FC na Home Boys FC dhidi ya
Ufukunyungu FC
Mashabiki wa soka na wadau wa michezo wameendelea
kuhamasishwa kujitokeza kwa wingi katika Uwanja wa Mwabenda ili kushuhudia
vipaji vya vijana vinavyoendelea kuibuliwa kupitia mashindano hayo.
Mashindano ya NIACHEKONA CUP 2026 yameandaliwa na mdau
wa michezo Paul Daud Augustino maarufu MC NIACHEKONA kwa ufadhili wa shirika la
Lushu Foundation, yakiwa na lengo la kuibua vipaji vya vijana, kuimarisha amani
na kukuza michezo katika jamii.
Kwa mawasiliano ya huduma za ushereheshaji wa shughuli
mbalimbali, matangazo na matukio ya kijamii, MC NIACHEKONA anapatikana kupitia
namba 0757 267 738.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


Post a Comment