Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga linawashikilia watu
75 kwa tuhuma za kufanya vurugu, kuwajeruhi watumishi wa umma pamoja na
kushiriki vitendo mbalimbali vya uhalifu katika Kijiji cha Sanjo, Kata ya
Idukilo, Wilaya ya Kishapu.
Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Shinyanga, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Janeth Magomi,
amesema matukio hayo yalitokea kati ya Mei 28 na Juni 1, 2026 wakati watumishi
wa umma walipokuwa wakitekeleza majukumu yao katika eneo hilo.
Amesema watuhumiwa hao wanadaiwa kushiriki katika
vitendo vya uvunjifu wa amani vilivyosababisha baadhi ya watumishi wa umma
kujeruhiwa pamoja na kuathiri utekelezaji wa shughuli mbalimbali za serikali
katika eneo husika.
Kamanda Magomi amesema Jeshi la Polisi lilifanya
operesheni maalum kufuatia matukio hayo na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao
ambao kwa sasa wanaendelea kuhojiwa huku uchunguzi ukiendelea kubaini ushiriki
wa kila mmoja wao.
Amesisitiza kuwa Jeshi la Polisi halitavumilia vitendo
vya uvunjifu wa sheria na kwamba hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya
yeyote atakayebainika kuhusika na matukio hayo.
Aidha, amewataka wananchi kuendelea kushirikiana na
vyombo vya ulinzi na usalama kwa kutoa taarifa za wahalifu na kuepuka kushiriki
katika vitendo vinavyoweza kuhatarisha amani na usalama wa wananchi.
Kamanda Magomi amebainisha kuwa baada ya kukamilika
kwa uchunguzi, watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma
zinazowakabili kwa mujibu wa sheria.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment