" RIDHIWANI AIPONGEZA TEA, ATAKA WANANCHI WAFAHAMU MAFANIKIO YA ELIMU

RIDHIWANI AIPONGEZA TEA, ATAKA WANANCHI WAFAHAMU MAFANIKIO YA ELIMU

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete, ameipongeza Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) kwa huduma mbalimbali inazotoa kwa wananchi na kuitaka kuongeza juhudi za kuelimisha umma kuhusu hatua na mafanikio ya Serikali katika kuboresha sekta ya elimu nchini.

Ridhiwani alitoa pongezi hizo alipotembelea banda la Mamlaka ya Elimu Tanzania katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma, ambapo alipata fursa ya kujionea huduma na shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na taasisi hiyo.

Akizungumza alipotembelea banda hilo la TEA, Ridhiwani alisema taasisi hiyo ina mchango mkubwa katika maendeleo ya elimu nchini kupitia usimamizi wa Mfuko wa Elimu wa Taifa, hivyo ni muhimu wananchi wakaendelea kupata taarifa sahihi kuhusu miradi na mafanikio yanayotekelezwa kwa manufaa yao.

Kwa upande wake, Afisa Uhusiano na Mawasiliano wa Mamlaka ya Elimu Tanzania, Eliafile Solla, alisema ushiriki wa TEA katika maadhimisho hayo unalenga kutoa elimu kwa wananchi kuhusu majukumu na shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na mamlaka hiyo kupitia Mfuko wa Elimu wa Taifa.

Ametaja majukumu makuu mawili yya TEA ambayo ni kutafuta rasilimali fedha na vifaa kutoka kwa wadau mbalimbali wa maendeleo na kisha kugawa rasilimali hizo katika shule na taasisi za elimu kwa lengo la kuboresha miundombinu ya kufundishia na kujifunzia nchini.

“Tunatumia maonesho haya kuwafikia wananchi moja kwa moja ili waelewe namna TEA inavyoshirikiana na wadau mbalimbali katika kuimarisha sekta ya elimu kwa kutoa rasilimali zinazosaidia ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya elimu pamoja na upatikanaji wa vifaa vya kujifunzia na kufundishia,” amesema Solla.

Ameongeza kuwa watumishi wa TEA walioshiriki maonesho hayo wamejipanga kutoa elimu kwa wananchi wanaotembelea banda hilo, sambamba na kuendelea kutekeleza jukumu la kutafuta rasilimali fedha na vifaa vitakavyosaidia kuimarisha juhudi za Serikali za kuboresha mazingira ya elimu nchini.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post