
Serikali imetangaza msimamo mkali dhidi ya mipango ya maandamano haramu yasiyo na kibali na kubainisha kuwa haitamfumbia macho wala kumuonea huruma mtu yeyote anayehusika katika kipindi hiki.
Akitoa taarifa hiyo bungeni jijini Dodoma leo Juni 26, 2026, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, amefichua kuwa tayari Jeshi la Polisi limekamata watu kadhaa na linatarajia kuanza kuwahoji ili kuchukua hatua stahiki.
Hatua hii imekuja baada ya Mbunge wa Dodoma, Pascal Chinyele, kuomba mwongozo wa Spika kwa kutumia Kanuni ya Kudumu ya 79 akitaka ufafanuzi wa serikali kuhusu matishio ya maandamano yanayosambaa kwenye mitandao ya kijamii.
Katika kukabiliana na matishio hayo ya uvunjifu wa amani, serikali imepiga marufuku mikutano yote ya hadhara ya vyama vya siasa nchini.
Waziri Katambi amemuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Camillus Wambura, kusitisha utoaji wa vibali vya mikutano ya hadhara ili kuruhusu vyombo vya usalama kujielekeza kikamilifu katika kudhibiti vitisho hivyo vinavyoratibiwa na baadhi ya watu mtandaoni.
Aidha, IGP Wambura ametakiwa kuwaelekeza Makamanda wa Polisi wa mikoa, wilaya, na polisi kata kuweka mikakati madhubuti ya ulinzi kwenye maeneo yao.
Sambamba na mikakati hiyo, Waziri Katambi ameagiza kufungwa kwa baadhi ya sehemu za starehe zenye viashiria vya uvunjifu wa amani, hususan katika maeneo ya Masaki na Oysterbay mkoani Dar es Salaam pamoja na maeneo mengine yanayohusika.
Ili kuimarisha usalama zaidi, serikali imetoa agizo la lazima kwa kila mgeni anayelala katika nyumba za kulala wageni kote nchini kuandikishwa kwenye daftari maalumu kwa kutumia Kitambulisho cha Taifa cha NIDA.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment