" SERIKALI YAWAHAKIKISHIA AMANI WANANCHI

SERIKALI YAWAHAKIKISHIA AMANI WANANCHI

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, amewahakikishia wananchi wa Tanzania kuendelea kufurahia amani na utulivu, huku akiwataka kushiriki shughuli za kiuchumi na maendeleo bila hofu.

Katambi ametoa kauli hiyo wakati wa hafla ya kufunga Mafunzo ya Awali Kozi Na. 6/2026 katika Chuo cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Chogo, wilayani Handeni mkoani Tanga, ambapo jumla ya askari 1,000 wamehitimu mafunzo hayo.

Amesema vyombo vya usalama vimejipanga kikamilifu kulinda amani ya nchi, ikiwa ni pamoja na kukabiliana na taarifa zinazosambazwa mitandaoni kuhusu maandamano yanayodaiwa kufanyika nchi nzima.

Kwa upande wake, Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, John Masunga, amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa kibali cha kuajiri askari hao 1,000 na kuthibitisha kukamilika kwa taratibu zote za ajira.

Mafunzo hayo yanayohitimishwa leo yanajumuisha wataalamu katika kada za Uzimaji Moto wa Kemikali, Maokozi ya Angani,nchi kavu na majini ambapo wanaume wapo 651 na wanawake 349.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254



Post a Comment

Previous Post Next Post