

Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya NIACHEKONA CUP 2026, Silas Elias Kadaso, amewaalika wananchi, wadau wa michezo na wapenda soka kujitokeza kwa wingi kushuhudia fainali ya mashindano hayo itakayofanyika Jumanne, Juni 23, 2026 katika Uwanja wa Mwabenda, Kata ya Solwa, Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.
Akizungumza baada ya kukamilika kwa michezo ya nusu
fainali, Kadaso amesema siku hiyo kutachezwa michezo miwili muhimu, ambapo
kuanzia saa nane mchana Duara FC itamenyana na Bulige FC katika mchezo wa
kusaka mshindi wa tatu.
Baada ya mchezo huo, kutafuata shughuli mbalimbali
zikiwemo burudani na hotuba ya mgeni rasmi, kabla ya kuanza kwa pambano kubwa
la fainali litakalowakutanisha Ufukunyungu FC kutoka Mjini Shinyanga na Kashishi
FC kutoka Kata ya Solwa, timu ambazo zimefuzu hatua hiyo baada ya kufanya
vizuri katika michezo ya nusu fainali.
Kadaso amesema mshindi wa kwanza wa mashindano hayo
atazawadiwa shilingi milioni moja na laki mbili (1,200,000), huku mshindi wa
pili akipata shilingi laki sita (600,000) na mshindi wa tatu akiondoka na shilingi
laki tatu (300,000).
Aidha, amesema kutakuwa na zawadi maalum kwa washindi
wa tuzo mbalimbali, zikiwemo mfungaji bora, mchezaji bora, golikipa bora pamoja
na timu yenye nidhamu zaidi, ambapo kila mshindi atapatiwa shilingi elfu 50,000.
Ameongeza kuwa maandalizi ya fainali yanaendelea
vizuri na kwamba kesho kutatolewa taarifa rasmi kuhusu mgeni rasmi
atakayehudhuria na kuzindua shughuli za siku ya fainali.
Mashindano ya NIACHEKONA CUP 2026 yameandaliwa na Paul
Daud Augustino maarufu MC NIACHEKONA kwa ufadhili wa Shirika la Lushu
Foundation, yakilenga kuibua vipaji vya vijana, kukuza michezo na kuimarisha
mshikamano wa jamii.
Kwa huduma za MC, matangazo na ushereheshaji wa
matukio mbalimbali, wasiliana na MC NIACHEKONA kupitia namba 0757 267 738.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment