" WAISLAMU RUVUMA WATOA WITO WA KULINDA AMANI, WAONYA DHIDI YA VIASHIRIA VYA UVUNJIFU WA AMANI

WAISLAMU RUVUMA WATOA WITO WA KULINDA AMANI, WAONYA DHIDI YA VIASHIRIA VYA UVUNJIFU WA AMANI


Na: Osama Mohamedi– SongeaMamia ya waumini wa dini ya Kiislamu mkoani Ruvuma wameadhimisha Mwaka Mpya wa Kiislamu 1448 Hijria kwa kufanya maandamano ya amani katika mitaa mbalimbali ya Manispaa ya Songea, huku viongozi wa dini wakitoa wito wa kuendelea kulinda tunu ya amani, haki, umoja na maridhiano na kuonya dhidi ya viashiria vya uvunjifu wa amani vinavyojitokeza kupitia mitandao ya kijamii na baadhi ya makundi.Maadhimisho hayo, yaliyobeba kaulimbiu ya "Amani, Haki, Umoja na Maridhiano," yaliwakutanisha viongozi wa dini, Serikali na mamia ya Waumini walioonyesha mshikamano wao kwa kufanya maandamano ya utulivu kabla ya kushiriki ibada na mkutano maalumu wa kutoa ujumbe wa amani kwa jamii.Akizungumza katika hafla hiyo, Sheikh wa Mkoa wa Ruvuma, Ramadhani Mwakilima, alisema kaulimbiu ya mwaka huu imekuja wakati muafaka kutokana na mazingira yanayoonyesha viashiria vinavyoweza kuhatarisha mshikamano wa taifa, akiwataka Watanzania kuendelea kuwa walinzi wa amani kwa kuepuka vitendo vya uchochezi na kutatua tofauti zao kwa njia za mazungumzo.Alisema Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) litaendelea kushirikiana na Serikali katika kuhamasisha wananchi kudumisha utulivu na mshikamano, huku akisisitiza kuwa maendeleo ya taifa hayawezi kupatikana bila kuwepo kwa amani.Sheikh Mwakilima pia aliwahimiza Waislamu kushiriki kikamilifu katika uchaguzi wa viongozi wa BAKWATA unaoendelea kwa kufuata taratibu zilizowekwa, akisema taasisi hiyo inaendelea kuhitaji viongozi wenye maadili na uwezo wa kuwatumikia Waumini na jamii kwa ujumla.Kwa upande wake, Katibu Tawala wa Wilaya ya Songea, Mtela Mwampamba, aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya, alisema msingi wa taifa lenye amani unaanzia katika malezi bora ya watoto, akiwataka wazazi kuacha dhana kwamba kuwafundisha watoto kufanya kazi za nyumbani ni adhabu.Alisema kuwajengea watoto ujuzi wa maisha, nidhamu na uwajibikaji ni sehemu ya kuwaandaa kuwa wananchi wenye kujitegemea na wenye mchango chanya katika maendeleo ya taifa.Aidha, aliipongeza BAKWATA Mkoa wa Ruvuma kwa kuendelea kulea vijana wenye uwezo wa kujenga hoja na kuelimisha jamii, akisema vijana hao ni rasilimali muhimu katika kuhamasisha maendeleo na matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii badala ya kueneza chuki na migawanyiko.Naye Mwenyekiti wa Vijana wa BAKWATA Mkoa wa Ruvuma, Sheikh Abdallah Ibn Abdallah Mpenda, aliwataka vijana kutambua kuwa wao ndiyo nguvu ya taifa na kwamba wanapaswa kutumia vipaji na uwezo wao kujenga familia, jamii na nchi badala ya kukubali kutumiwa katika vitendo vya vurugu au uharibifu.Alisema vijana wanapaswa kuwa mstari wa mbele katika kueneza ujumbe wa amani na maendeleo, huku wakitumia mitandao ya kijamii kwa shughuli zenye manufaa badala ya kuruhusu kutumiwa na watu wenye nia ya kuvuruga utulivu wa taifa.Maadhimisho ya Mwaka Mpya wa Kiislamu 1448 Hijria yalihitimishwa kwa dua maalumu ya kuliombea taifa liendelee kuwa na amani, umoja, maridhiano na maendeleo, huku viongozi wa dini wakisisitiza kuwa amani ni msingi wa maendeleo na wajibu wa kila Mtanzania kuilinda.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post