
Maafisa usafirishaji katika Kituo cha Mkongwe kilichopo Mtaa wa Kambarage Sokoni, Manispaa ya Shinyanga, wamepewa elimu ya usalama barabarani na kutakiwa kuacha tabia ya kuegesha vyombo vyao vya usafiri kwenye maeneo ya kona wakati wakisubiri abiria.
Elimu hiyo imetolewa na Askari Polisi kutoka Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga, Sajenti David Ndimila, ambaye amesema baadhi ya waendesha vyombo vya usafiri wamekuwa wakiegesha katika maeneo ya kona na kusababisha kupungua kwa upana wa barabara pamoja na kuhatarisha usalama wa watumiaji wengine wa barabara.
Sajenti Ndimila amewataka maafisa hao kuzingatia taratibu za usalama barabarani kwa kuhakikisha wanachagua maeneo sahihi ya kusimama wanapokuwa wakisubiri abiria, ili kuepuka kusababisha msongamano na ajali zinazoweza kuzuilika.
Amesisitiza kuwa usalama wao wenyewe unapaswa kuwa kipaumbele wakati wanapotekeleza majukumu yao, huku akiwakumbusha kuwa elimu ya usalama barabarani ni muhimu kuendelea kutolewa kwa abiria na madereva ili kupunguza ajali na madhara yanayotokana na uzembe barabarani.
Aidha, amewakumbusha maafisa hao kuhakikisha vyombo vyao vinakuwa na nyaraka muhimu ikiwemo leseni halali za udereva pamoja na bima za vyombo vyao, ili waweze kufanya shughuli zao kwa kuzingatia sheria.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254





Post a Comment